MSIGWA: KITUO KIKUBWA CHA KAHAWA KUJENGWA NCHINI
Dar es salaam - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Shirika la Kahawa Barani Afrika (Inter-African Coffee Organisation- IACO) limeahidi kujenga kituo kikubwa nchini cha utafiti wa kahawa kitakacho hudumia bara la Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo march Mosi jijini Dar es salaam juu ya mafanikio mbalimbali ya serikali ya awamu ya sita tangu kuingia madarakani amesema ujenzi wa kituo hicho pamoja na mambo mengine utaongeza fursa mbalimbali ikiwemo kuongeza wataalamu na kuzalisha ajira.
Alisema ujezni huo unakuja kufatia
Kufanyika kwa Mkutano wa mkubwa Kahawa barani Afrika ambao Tanzania tulikuwa mwenyeji na kuandaliwa kwa kushirikiana na IACO mapema mwezi February mwaka huu.
Amesema ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarajiwa kujengwa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ilipo Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa lengo la kuiongezea nguvu lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa kahawa yenye ubora.
Msigwa aliongeza kuwa moja ya azimio ya mkutano huo ni kuwa kufikia 2035 angalau asilimia 50 ya kahawa inayozalishwa barani Afrika na kuuzwa nje iwe imesindikwa na kuongezwa thamani ndani ya bara la Afrika
No comments