Breaking News

BARAZA LA USHAURI DSM LAPITISHA BILIONI 848 RASIMU YA BAJETI 2025/2026

Baraza la Ushauri la Mkoa wa Dar es Salaam (RCC) limepitisha rasimu ya bajeti yake ya mapato na matumizi ya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 848 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 itakayotoa dira ya utoaji huduma muhimu za kijamii pamoja na matumizi ya mishahara kwa watumishi

Akizungumza wakati wa kuwasilisha rasimu hiyo ya bajeti Februari 28, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ambaye ni mwenywkiti wa baraza hilo amesema kuwa rasimu hiyo ya mapendekezo ya mapato na matumizi kama Mkoa wataiwasilisha kwenye kamati za bunge na mamlaka zote husika ili isaidie kuboresha na kuimarisha huduma za Jamii
Aidha akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika kabla ya RCC Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amesema ni muhimu kuendelea kuimarisha barabara mkoani humo ambapo ameagiza miradi yote ya DMDP 2 ambayo imesainiwa wakandarasi wawe kazini na kwamba wanaunda mfuko maalum wa barabara kusimamia barabara zote.

Katika Mkutano huo wa bodi ya barabara Mkoa wa Dar es salaam wabunge mkoani humo wameshauri uwepo wa mpango maalum wa kuwezesha kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwani changamoto ya barabara imekuwa kubwa kwa wananchi kuliko hata hata changamoto za elimu na afya.
Hata hivyo waziri wa mawasiliano na tekinolojia ya habari ambae ni Mbunge jimbo la ukonga Jery Silaa amesema licha ya kuwa kazi kubwa inafanywa na serikali kuboresha huduma ni muhimu kwa serikali mkoani humo kuongeza kasi kwenye ujenzi wa barabara

Mwisho Vikao vyote RCC na Bodi ya Barabara ya Mkoa vilihudhueiwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila, Kamati ya Usalama ya Mkoa, Mameya , Wakuu wa Wilaya zote, Wabunge, Watalaam wa Barabara, Vyama vya Siasa pamoja na Sekretarieti ya Mkoa



No comments