RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA AWASILI NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI ZA EAC NA SADC
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb.) amempokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa ambaye amewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments