WAZIRI MAJALIWA MGENI RASMI UZINDUZI WA MRADI WA HALI YA HEWA WA SOFF TANZANIA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mradi wa Hali ya Hewa wa SOFF Tanzania utakafanyika tarehe 21 Januari, 2024, katika Ukumbi wa Hoteli ya Midland Inn View, Dodoma
Zaidi kuhusu mradi MRADI WA SYSTEMATIC OBSERVATIONS FINANCING FACILITY (SOFF)
SOFF ni Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa kwa Nchi zinazoendelea na Nchi za Visiwa vidogo.
Kaulimbiu ya Mradi huu ni: "Taarifa za Hali ya Hewa kwa Hatua Stahiki
Lengo la Mradi huu ni: Kuimarishaji huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa ili kulinda maisha ya watu na mali. Faida za Mradi huu kwa nchi: Mradi huu wa SOFF utasaidia kuboresha mahitaji ya uboreshaji zaidi miundombinu ya uangazi wa hali ya hewa na kuhakikisha kwamba tunakidhi mahitaji ya wadau wa Kitaifa na Kimataifa.
Sambamba na kuwezesha Taifa kutekeleza majukumu ya Kimataifa ya uangazi na ubadilishanaji wa data za hali ya hewa kwa kuboresha miundombinu ya uangazi na teknolojia za kisasa zinazohitajika. Pia, mradi wa SOFF utakuwa ni kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla, ikizingatiwa kwamba data sahihi za hali ya hewa ndicho kiini cha taarifa sahihi za hali ya hewa zinazohitajika katika kuokoa maisha ya watu na mali zao na kuchochea ukuaji endelevu. Mradi wa SOFF utatekelezwa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2027.
Washiriki wa hafla hiyo ni wadau wa huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi zinazochangia katika mfuko wa SOFF, Wizara, Taasisi za serikali, Taasisi binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu, Washirika wa Maendeleo na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Hafla hiyo imeandaliwa na Wizara ya Uchukuzi kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Taasisi ya Hali ya Hewa ya Denmark (Danish Meteorological Institure-DMI) itfanyika tarehe 21 Januari, 2025, katika Ukumbi wa Hoteli ya Midland Inn View, Dodoma
No comments