RC CHALAMILA: MAANDALIZI YA KUPOKEA UGENI WA MARAIS WA AFRIKA YANAENDELEA VIZURI
Wakati Tanzania ikiwa inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Marais wa Afrika unaotarajia kufanyika Januari 27 na 28 mwaka huu kujadili masuala ya Nishati Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea maeneo muhimu kuelekea mkutano huo na kueleza kuwa maandalizi yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Akizungumza mara baada kumaliza ziara hiyo RC Chalamila amesema amesema lengo la ziara hiyo ambayo imeanzia eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere ni hadi katika ukumbi wa Karimjee na JNICC ni kikagua barabara na usafi wa mazingira sambamba na kujionea pia maandalizi ya kufunga taa za kisasa zitakazosaidia kuhakikisha jiji linakua na mwanga wa kutosha.
Katika ziara hiyo pia RC Chalamila amesisitiza suala la usafi na kupendezesha Jiji ambapo amewataka wananchi kuhakikisha kuwa usafi unafanyika sio kipindi hiki cha ugeni bali iwe ni utamaduni wa kila siku sambamba na kuwepo na bustani za miti na maua tuendelee kuwa kivutio kwa mikutano mingine mbalimbali ya kimataifa na uwekezaji
Katika hatua nyingine RC Chalamila ameongeza kuwa kufatia ugeni wa vingozi utakaokuwepo nchini baadhi ya barabara zitafungwa ili zitumike na wafanyabiashsara na wajasiriamali wa kitanzania kuonesha bidhaa mbalimbali za kiutamaduni zinazoitambulisha Tanzania kwenye mataifa mbalimbali yanayoshiriki mkutano huo na msisitizo kwa wananchi kuwa suala la kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini liendelee ili tuendele kuwa kitovu cha amani na kuvutia wawekezaji.
Aidha RC Chalamila pia amezungumzia suala la magari kupaki kwenye hifadhi za barabara yaani road reserve ambapo amesema hilo ni kosa kisheria hivyo ameitaka TANROAD kushughulikia tatizo hilo linalosabisha hifadhi za barabara zisitumike vibaya
No comments