WAANDISHI WA HABARI MSIPOKEE BAHASHA NI UTUMWA - PADRE MASENGE
Dar es salaam - Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo la Dar es salaam na Tumaini Media, Padri Joseph Masenge Ametia wito kwa waandishi wa waandishi wa Habari nchini Kutumia karamu zao kueneza ujumbe wa mwenyezi mungu na Amani njema wasiwe waandishi wa Habari wa Bahasha.
Akizungumza katika ibada iliyowaleta pamoja waandishi wa habari katoriki mkoa wa Dar es salaam amesema uandishi wa habari ni moja ya taaluma ambayo imekuwa mkumbozi kama itatumika vizuri na kwa weredi hivyo Tumuombe Mt. Paulo atuombe tusiwe waandishi wa Habari wale wa Bahasha Bali tuwe waandishi wa Habari wa kupeleka ujumbe wa kweli.
"Changamoto moja wapo ambayo imewakumba waandishi wa Habari wengi kwa sasa ni kupuuza Yale maadili ya Uandishi wa Habari kwa kuanza kuyaweka pembeni na tunakimbilia Habari ambazo zina Bahasha". Alisema Padre Masenge
No comments