Breaking News

RC CHALAMILA AONGOZA WANANCHI ILALA ZOEZI LA KUFANYA USAFI

- Asema Tanzania inaingia kwenye historia nyingine ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Marais wa Afrika

- Atoa taarifa ya kufungwa kwa baadhi ya barabara siku chache ambazo ugeni utakuwa katika Mkoa huo

Dar es salaam - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Januari 25, 2025 ameongoza mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ilala kufanya usafi kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwl JK Nyerere barabara ya Terminal One kuelekea mjini (City centre) ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya ugeni mkubwa wa Marais wa Afrika ambao wanatarajia kuwasili nchini kuanzia leo.

Akizungumza mara baada ya kuanza kwa zoezi hilo RC Chalamila amesema Tanzania inaingia katika historia ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa utakao wakutanisha Marais wa nchi za Afrika kujadili masuala ya Nishati ambao utafanyika tarehe 27-28/01/2025 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. 
Alisema Mkutano huo unakuja na fursa nyingi za kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla ambapo Mhe Mkuu wa Mkoa amewataka wakazi wa Mkoa huo kuzitumia vizuri fursa hizo.

Aidha RC Chalamila amesisitiza umuhimu wa kuweka Mkoa katika hali ya usafi nyakati zote za ugeni huo ukiwa katika mkoa wetu na mara baada ya kuondoka tabia ya usafi iwe ni utamaduni wa kila siku kwa kila mtu.
Vilevile RC Chalamila amesema kwa kuwa ugeni huo ni mkubwa baadhi ya barabara zitafungwa kwa siku chache ambazo ugeni huo utakuwepo katika Mkoa wetu.

Zoezi hilo ambalo pia limeudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo kufanya usafi akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Wilaya hiyo. 





No comments