ROBO FAINALI YA KHIMJI SUPER CUP 2025 YAFANA JIJINI DAR
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam - Mashundani ya mpira wa miguu Kimji super Cup yaliyochezwa kwenye kiwanja cha Garden Ilala Dar es salaam,kati ya timu ya Young stars na Sirros timu ya Sirros imeibuka na ushindi wa mabao mawili dhidi ya moja.
Mahasimu hao waliingia uwanjani huku kila timu ikionyesha tambo kwa mwenzake, ambapo pambano lilikuwa ni zuri katika hatua ya robo fainali yenye kusisimua mioyo ya wapenzi mbalimbali waliohudhuria kiwanjani hapo.
Hayo yamebainishwa Januari 24,2025 j ijini Dar es salaam mgeni rasmi katika michezo huo Masau Bwire amesema ni jambo jema kwa vijana kujiegemeza katika michezo ambapo huletamahusiano mazuri miongoni mwa vijana wa kitanzania
"Tumshukuru sana Diwani kwa kuandaa mashindano haya ambayo yanaleta chachu katika makundi ya vijana na wazee ambao ni wapenda soka, katika mashindano haya nategemea nitawapata baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kucheza timu yetu ya JKT," amesema Bwire.
Aidha Bwire amesema kuwa michezo huleta fursa mbalimbali ,urafiki, umoja, ushirikiano hivyo ninawashukuru wachezaji na wapenzi waliojitokeza kwenye pambano hili. Serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imejipambanua katika kudumisha suala la michezo.
Mashindano hayo yameandaliwa na Diwani wa Ilala,Saad Khimji kwa nia ya kuwashirikisha vijana wapenda soka katika kuleta afya, furaha na mahusiano mema miongoni mwao kuondoa dhana za kutegemea njia za mkato katika utafutaji wa maisha ambapo kutakuwa na Zawadi mbalimbali ikiwemo kujinyakulia kikombe,medal ya silver pamoja na jezi mbalimbali.
No comments