Breaking News

11 MBARONI KWA TUHUMA ZA UHALIFU DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 Kwa tuhuma mbali mbali za kihalifu ikiwepo kosa la uhujumu uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi Bado linaendelea kusimamia  mkakati wa kuzuia vitendo vyao kihalifu  na kuhakikisha dar es salaam inaendelea kuwa salama.

Amesema kufuatia hali hiyo jeshi la polisi lilikuwa linafanya ufuatiliaji mkali mwezi Septemba mwaka huu na kufanikiwa kumkamata Twaha Salum miaka 53 na wenzake Saba.

Amesema Twaha na wenzake na wenzake Saba wanashikiliwa na polisi Kwa tuhuma za kuhujumu na kuharibu miundombinu ya bomba la gesi kampuni ya Oryx linalosafirisha gas kutoka bandari ya Dar es Salaam.

"Watuhumiwa hawa wamehojiwa Kwa Kina, ushahidi umekusanywa na watafikishwa kwenye mamlaka zingine Kwa hatua zaidi za kisheria", amesema Muliro.

Amesema katika hatua nyingine jeshi la polisi Kanda Maalum linamshikilia dereva Daud Matola (50) gari namba T882 DQK aina ya Benz na tela T.884 mkazi wa Kimara Dar es Salaam na wenzake wawili kwa tuhuma za wizi wa madini aina ya coppercathode yaliyokuwa yakisafirishwa kutoka nchini Kongo kwenda bandari ya Dar es Salaam.

Muliro amesema baada ya tukio watuhumiwa walilitekeleza gari hio.

Aidha amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa na kuahidi kutokuwa na huruma Kwa wahalifu na kuendelea kuwashughulikia vikali lakini kwa mujibu wa sheria 

No comments