Breaking News

WAZIRI JAFO - BRELA ENDELEENI KUWA WAWEZESHAJI WAFANYABIASHARA KURASIMISHA BIASHARA ZAO

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw.Godfrey Nyaisa akitoa maelezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo namna Wakala wa Usajili wa Biashara Leseni (BRELA) inavyofanya kazi zake mapema leo Septemba 9,2024 ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo akionyeshwa namna mfumo mbalimbali inavyofanya kazi katika ziara yake aliyoifanya mapema leo Septemba 9,2024 ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA, Prof. Neema Mori akimpokea waziri Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo mara baada ya kuwasili ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw.Godfrey Nyaisa (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA, Prof. Neema Mori (kushoto) mara baada ya ziara ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dokta. Selemani Jafo amewaelekeza watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara Leseni (BRELA) kuwa wawezeshaji wa Wafanyabiashara kwa kuwasaidia katika kufanikisha kurasimisha biashara zao na siyo kuwa kikwazo. 

Akizungumza mapema leo Septemba 9,2024 mara baada ya kumaliza ziara aliyoifanya ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea utendaji kazi na kujifunza namna Wakala inavyotoa huduma za Sajili mbalimbali. 

Alisema napenda kutoa rai wabunifu wote nchini kulinda bunifu zao kwa kuzisajili kisheria ili zisichukuliwe na watu wengine na kujinufaisha nazo bila kufuata utaratibu wa kisheria kwani bunifu nyingi zinachukuliwa na watu wengine uku wale wabunifu halali hawanufaiki na chochote kwa kuwa hawakuzisajili.

“Ninatoa wito kwa Watanzania wabunifu wote kusajili bunifu zenu kupitia BRELA maana taasisi hii inakazi ya kulinda haki za ubunifu ili kuwawezesha kufaidika na jitihada za ubunifu na hatimaye kuongeza kipato kwa wabunifu na taifa kwa ujumla” Alisema Dkt. Jafo.

Ameeleza kuwa, Tanzania imesaini mikataba na nchi mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na SokoHuru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika maeneo hayo yote Watanzania wanashiriki katika biashara mbalimbali hivyo kuna haja kubwa ya wabunifu kutambua haki zaoili zisichukuliwe na wenzetu hivyo niwaombe Watanzania kusajili bunifu zao.

Aidha, amewataka kutumia kanuni na sheria kusaidia biashara kwenda mbele na sheria ambazo zinakwamisha ziwasilishwe ili ziweze kufanyiwa maboresho kwamba nimuhimu kuelewa jukumu la BRELA ni kujenga misingi na mazingira mazuri ya biashara.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA, Prof. Neema Mori, amesema kuwa BRELA imedhamiria kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini yanakuwa bora zaidi kwa kuwawezesha, kuwarahisishia na kutoa usaidizi wa karibu kwa wafanyabiashara wanapo rasimisha biashara, kutoa elimu pamoja na kuwahusisha wadau mbalimbali ili wajue namna.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw.Godfrey Nyaisa amesema kuwa kwa sasa sera ya miliki ubunifu inaelekea kupitishwa na baadae kuwa na sheria ambayo itasaidia ongezeko kubwa la maombi ya ulinzi wa bunifu hizo ambapo kuna jitihada ambazo BRELA inaendelea nazo katika kuhakikisha elimu ya miliki bunifu inafahamika kuanzia ngazi ya shule ya za msingi hadi vyuo vikuu.

Mbali na jukumu la kusajili miliki ubunifu na utoaji wa hataza amesema kuwa BRELA inatoa ufadhili wa Shahada ya Uzamili ya Miliki Ubunifu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaamkwa watu watano kila mwaka ambapo elimu hii mtu atakayoipata itasaidia katika ukuaji wa sekta ya miliki ubunifu nchini

No comments