Breaking News

MBUNGE WA LINDI MHE. HAMIDA ABDALLAH AMJULIA HALI KALUME HOSPITALI YA MUHIMBILI

Mheshimiwa Hamida Mohammed Abdallah akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) muda mfupi baada ya kutoka kumuona Kalume hospitali ya Taifa ya Muhimbili Septemba 9, 2024
Mama wa Kalume Salima Nasoro Kalume (kushoto) akisalimiana na Mbunge Hamida Mohammed Abdallah mara baada ya kuwasili hospitali ya Taifa ya Muhimbili Septemba 9, 2024

Pichani Mheshimiwa Hamida Mohammed Abdallah (katikati) akiwa na Mama wa Kalume Salima Nasoro Kalume na baadhi ya Wanachama wa Dar es salaam City Press Club (DCPC) muda mfupi baada ya kutoka kumuona Kalume hospitali ya Taifa ya Muhimbili Septemba 9, 2024

Dar es salaam;
Mbubge wa Lindi Mjini, Mhe. Hamida Mohammed Abdallah amemtembelea na kumuona Kalume Ally Kalume (41) aliyelazwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu tangu Agosti 24, 2024.

Kalume anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama sehemu mbalimbali za mwili amelazwa wodi ya Sewahaji.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumtembelea Kalume, September 9, 2024, Mhe. Hamida alifurahi kumuona Kalume akiendelea vyema na matibabu ya kibingwa yanayotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

"Nimefurahi kukuona ndugu yangu, nakuahidi kuwa na wewe katika kipindi chote cha maumivu yako, nimetoka Dodoma nikaona nisiende Lindi hadi nije kukuona, pole sana ndugu yangu"

Aidha, Amesema kuwa lengo la kufika hapo ni kuja kumuona mpiga kura wake huyo na yeye kama mbunge wa Lindi Mjini watahakikisha wanampa faraja ambayo ameikosa kwa miaka zaidi ya 20. 

"Naaamini kwa opereseni hizi anazofanyiwa atarudisha furaha yake ambayo ameikosa kwa muda mrefu,

Hadi sasa nafurahi kumuona akiwa amevaa shati la ukubwa wake, wakati zamani alikuwa akivaa shati lililomzidi," amesema Mhe. Hamida Abdallah.

Hadi sasa tayari ameshafanyiwa operesheni ya kwanza katika sehemu za uso na mgongoni huku akisubiri operesheni nyingine sehemu ya makalio na kwenye mapaja.

Hadi sasa matibabu ya Kalume yanaratibiwa na Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es salaam (DCPC) kwa kushirikiana na ndugu na  jamaa ambapo zoezi la ukusanyaji wa fedha za matibabu zikiratibiwa na Kalunde Saidi.

"Watu wote watakaoguswa kusaidia kuchangia Mgonjwa wanaweza kutuma kiasi chochote cha pesa kupitia kwa Mratibu Mkuu wa zoezi hili Bi. Kalunde Saidi kupitia namba ya Mtandao wa Airtel 0684695698",  Amesema Bi Careen Mgonja ambaye ni mratibu msaidizi wa zoezi hilo la kurejesha tabasamu kwa Kalume Ally Kalume.

No comments