Breaking News

WASANII WAFANYA TAMASHA LA KUWAENZI WASANII WENZAO WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI

Wasanii wa Maigizo (Bongo Muvie), Waimbaji, Watangazaji pamoja na wachekeshaji leo septema 7,2024 wameungana katika tukio kubwa la kuwakumbuka na kuenzi mchango wa wasanii wenzao kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki. 

Akizungumza katika viwanja vya Leaders jijini Da es salaam msanii Ivon Cherry maarufu kama (Monalisa) amesema lengo kubwa la kufanya kumbukizi hiyo ni kutambua na kuenzi mchango wa wasanii hao wote katika kukuza pamoja na kutangaza sana yetu ndani na nje ya nchi.

"Leo tunakutana hapa kwa lengo la kuenzi mchango mkubwa wa wenzetu ambao kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki ambao kwa kutambua mchango wao mkubwa katika sanaa katika kuhakikisha Sanaa yetu inakuwa ndani na nje ya nchi yetu". Alisema Monalisa.

Alisema kwa kuzingatia mchango wao katika kukuza Sanaa pamoja na kuitangaza ndani na nje ya nchi sisi kama wasanii tumeona ni vizuri kuandaa kumbukumbu hii ili kutambua mchango wao umuhimu katika Sanaa yetu.

Kumbukumbu hiyo umeandaliwa na Taasisi ya mama ongea na mwanao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka katika nyanja ya burudani, Maigizo na utangazaji. 

No comments