Breaking News

ASKOFU KUTTA: TUTASHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUWALETA MAENDELEO WANANCHI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Catholic church Jimbo la Tanzania, Dokta Elibariki Philip Kutta amesema kanisa hilo litashirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo watanzania

Akizungumza kijijini Mlali wilayani Kongwa muda mfupi mara baada ya Misa takatifu ya kumsimikwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa hilo Nchini amesema pamoja na kutoa mafundisho ya Dini pia kanisa hilo litashirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi. 

"Tutashirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa tunasaidia wananchi hususani waishio vijijini kuwaletea maendeleo wananchi hususani huduma za afya, elimu na maji". Alisema Askofu Kutta.
Alisema kanisa linatambua hazma ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hasa waishio vijijini hususani katika sekta ya maji na Afya. 

Akitolea mfano changamoto ya upatikanaji wa maji ameeleza kuwa shida ya Maji inasababisha Wananchi kutumia mda mwingi kutafuta maji hivyo kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushindwa kuhudhuria ibada na mafundisho ya dini hususani wakati wa kiangazi 

Ameongeza anatamani kuona maji yanamfuata mwananchi na sio mwananchi anafuata maji na kila nyumba katika Wilaya hiyo inakuwa na bomba la maji na ndoto ya mradi huo itanzia kijiji cha Mlali wilayani Kongwa 
Katika hatua nyingine askofu Kutta pia ametoka wito kwa wananchi hususani wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea katik maeneo mengi nchini. 

"Wakazi wa Mkoa wa Dodoma tujitokeze kushiriki kikamilifu katika  mchakato wa uwandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linalotaraji kuanza Oktoba 25 mpaka Novemba 1 mwaka huu". Alisema Askofu kutta. 

Kwa upande wake Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Catholic church Duniani, Mark Hervland Kanisa liko tayari  kushirikiana na Dokta Elibariki Philip Kutta katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii hususani ujenzi wa Miundombinu ya Maji safi na tiririka. 

"Tangu nimewasili nchini na kutembelea maeneo mbalimbali nimeona dhamira ya dhati ya Askofu Kutta napenda kumwahaidi kuwa tutashirikiana nae katika kuanzisha miradi a huduma za kijamii ikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa michezo katika Kijiji cha Mlali wilayani Kongwa pamoja na ujenzi wa Zahanati ambapo miradi hiyo itakamika kwa wakati". Alisema Mhashamu Hervland. 






No comments