Breaking News

PINGAMIZI KWA MGOMBEA WA ADC LATUPWA WAJUMBE 197 KUAMUA JUNE 29, 2024

Dar es Salaam.
Wakati wapiga kura 197 wakitarajia kufanya uamuzi wa kikatiba kumchagua mwenyekiti mpya wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Kamati ya uchaguzi huo imesema pingamizi alilowekewa mmoja wa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti, Shabani Haji Itutu halijafuata kanuni za chama.

Itutu aliwekewa pingamizi na wanachama saba wa ADC, Ibrahim Pogora, Asha Milongea, Asha Mzee, Khadija Tambwe, Maisala Khamis, Doni Mnyamani na Halima Msumali wakidai ni mwanachama wa chama kingine cha upinzani.

Katibu wa kamati ya uchaguzi, Innocent Siriwa ameiambia Mwananchi Digital leo Ijumaa, Juni 28, 2024 kwamba wamepokea pingamizi hilo, lakini kwa mujibu wa kanuni za chama, kamati haitalifanyia kazi.

 

No comments