Breaking News

DOROTHY SEMU AJITOSA KUMRITHI ZITTO KABWE, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara na Waziri Mkuu kivuli wa chama hicho, Bi. Dorothy Semu akielekea makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya kiongozi wa chama hicho mapema leo February 18, 2024 jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara na Waziri Mkuu kivuli wa chama hicho, Bi. Dorothy Semu akionyesha mkoba wenye fomu ya kugombea mara baada ya kukabidhiwa rasmi makao makuu ya chama hicho mapema leo February 18, 2024 jijini Dar es salaam.

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara na Waziri Mkuu kivuli wa chama hicho, Bi. Dorothy Semu akisaini nyaraka mbalimbali  kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya kiongozi wa chama hicho mapema leo February 18, 2024 jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara na Waziri mkuu kivuli, Bi Dorothy Semu leo February 18, 2024 amechukua rasmi fomu  ya kugombea nafasi ya kiongozi wa chama hicho jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema anagombea nafasi hiyo ya Kiongozi wa chama hili kuendeleza dhima chama cha ACT Wazalendo ambayo imeibeba Kwa zaidi ya miaka kumi. 

"Nagombea nafasi hii ya Kiongozi wa chama kuendeleza dhima hiyo ambayo chama cha ACT Wazalendo ambayo imeibeba Kwa miaka kumi (10) sasa na matumaini inayotoa katika uongozi wa nchi hii, ninataka kuongoza ndoto hii ya ACT Wazalendo kufikia mabadiliko chanya ya kweli ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni" Alisema Bi. Semu.

Alisema katika kipindi cha miaka kumi ya kukitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali za uongozi ninataka kutumia uzoefu wangu na karama ya uongozi kuongoza jahazi hili la ACT Wazalendo kwenye kushika hatamu ya kuongoza Taifa hili.

Bi Semu aliongeza kuwa atahakikisha kuwa anaendeleza na kusimamia wajibu wa uwepo wa chama hiki katika vyama vingi vya siasa za ushindani umeleta tafsiri halisi ya nini maana ya chama shindani, tumekuwa ni chama ambacho siku zote tumeleta sera za kimapinduzi ambazo zitakwenda kubadilisha kabisa hali ya umaskini ya watu wetu

"Mimi ni mmoja ya wanaoamini katika wajibu mkubwa wa vyama shindani uwepo wa chama hiki katika vyama vingi vya siasa za ushindani umeleta tafsiri halisi ya nini maana ya chama shindani, tumekuwa ni chama ambacho siku zote tumeleta sera za kimapinduzi ambazo zitakwenda kubadilisha kabisa hali ya umaskini ya watu wetu" Alisema na kuongeza kuwa 

"Nitahakikisha kuwa anasimamia na kutengeneza Sera mbadala zenye tija lakini pia tumeendelea kujitofautisha na vyama vingine kwa kutoa siasa za masuala na kuendelea kuwa sauti kuu ya wanyonge na kututofautisha kabisa na kila chama ambacho kimewahi kutokea katika nchi hii, tunataka kuendelea kuwa kimbilio na sauti kuu ya Watanzania katika kutafuta maisha ya neema kwa kila Mtanzania" 

Bi Dorothy Semu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara na Waziri Mkuu kivuli katika kipindi cha miaka kumi ya utumishi wake ndani ya chama ameshika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Katibu wa sera na utafiti na sasa Waziri Mkuu Kivuli.


No comments