Breaking News

DKT. BITEKO MGENI RASMI MKUTANO WA WADAU WA UTAMADUNI NA SANAA

Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Utamaduni na  Sanaa utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024  ukishirikisha wadau  takribani  800 wa Tanzania Bara.

Akizungumza  katika mkutano na vyombo vya habari leo Februari 27,2024 jijini Dodoma  Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ameeleza kuwa  mkutano huo ni katika kuendelea kuimarisha sekta za Utamaduni na Sanaa nchini lengo ikiwa ni kujadili kwa pamoja mwenendo wa sekta hizo pamoja na kuziboresha.

"Kupitia mkutano huo wadau wa Utamaduni na Sanaa watapata wasaa wa kujengewa uwezo, kubadilishana uzoefu , kufahamiana, kuendesha mijadala yenye afya kwa ajili ya kubainisha changamoto zinazoikabiki Sekta na kuweka mikakati ya kuitatua pamoja na kuwatambua na kuwatunuku wadau waliofanya vizuri katika zekta hizo" ameongeza Katibu Mkuu Msigwa.

Amesema kuwa, walengwa wa Mkutano huo ni Taasisi zinazojishughulisha na Utamaduni na Sanaa, Taasisi za fedha, Kampuni za Bima, Washirika wa Maendeleo, Kampuni za Simu, Vyuo vya Elimu ya Kati na juu, Asasi za kiraia na Taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na urasimishaji wa kazi za Sanaa

No comments