Breaking News

MCHINJITA AJITOSA KUCHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI TAIFA

Dar es salaam
Leo ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza Zoezi la uchukuaji na rejeshaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha ACT Wazalendo ambapo hadi leo 16 February  2024 wanachama 25 tayali  huku nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Chama bado haijapata mgombea.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi, bwana Idrissa amesema mpaka kufikia leo  wagombea waliojitokeza kuchukua fomu za ni pamoja na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Massoud Othman ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa, huku Juma Duni Haji akitetea nafasi yake.

"Tangu kuanza rasmi kwa Zoezi hili ambalo lilifunguliwa rasmi Feb 14, mwitikio umekua mkubwa, ambapo Naibu Waziri Kivuli wa Nishati Isihaka Mchinjita ni miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu kugombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Taifa" Alisema Idrissa. 
Mapema Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu kugombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Taifa leo Feb 16, 2024, bwana Isihaka Mchinjita amesema miongoni mwa sababu zilizomfanya achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo ni pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujenga misingi imara ya kitaasisi ndani ya Chama na kupigania ujenzi wa demokrasia pana yenye maslahi ndani ya nchi ya Tanzania.

Alisema kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Kivuli wa Nishati niliwai kuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Lindi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na nimezitumikia nafasi hizo kwa uwezo mkubwa na anaamini mchango wake umeacha alama katika kutumikia chama chake.

"Nimezitumikia nafasi zangu zote kwa kadri ya uwezo wangu na imani yangu ni kuwa wanachama wenzangu watakaochukua nafasi hizi wataendelea kuzitumikia katika namna bora zaidi kwa maslahi ya chama chetu na Taifa kwa ujumla" Alisema Bw. Mchinjita.
Alisema chama tayali kimepiga hatua kubwa ya ukuaji ndani ya muda mfupi tangu kuasisiwa kwake nchini na miongoni mwa mambo yaliopiga hatua ni uimarishwaji wa muundo wake jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele

Chama cha ACT Wazalendo kilizindua zoezi la kuanza rasmi kutoa rasmi fomu Feb 14 na zoezi hilo linatarajiwa kufikia tamati Feb, 24 ambapo nafasi mbalimbali zitagombewa ikiwemo ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti, Ngome ya Vijana, Wajumbe wa kamati kuu, pamoja na Halmshauri Kuu. 

No comments