Breaking News

ACT WAZALENDO YATOA TATHIMINI ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU

Chama cha ACT Wazalendo kimesema licha ya kuhamasisha na kutoa kipaumbele kwa wanawake na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho bado mwako umekuwa hafifu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Joran Bashange amesema kushindwa kwao kujitokeza kunaweza kuwa na adhali mbambali ikiwemo kutokushiriki katika vikao vya maamuzi ikiwemo vile vinavyowahusisha Wanawake wenyewe. 

“Tangu kuanza kwa zoezi la uchukuaji fomu na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama ambalo limehitimishwa Jana ambapo wugombea nafasi 6 za juu za uongozi wa Chama Ngome Wanawake 15 tu ikilinganishwa na ngome ya Wazee waliojitokeza ni 30 hii inadhihirisha kuwa mwamko bado ni mdogo Kwa Wanawake” Amesema Bashange.

Alisema pamoja na chama kuandaa mazingira kwao ikiwemo kupitisha sera ya jinsia ikiwa ni hatua mahususi katika chaguzi zake Kikatiba na kikanuni ambapo kumekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia Wanawake kuingia kwenye vikao vya maamuzi.

Aidha Bashange aliongeza kuwa tangu kuanza jwa zoezi la kuchukua na kurejesha fomulililofikia tamati janasaa 10 alasili jumla wagombea 179 wamejitokesa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama. 

Alisema mara baada ya kumalizika kwa awamu hiyo zoezi litakalofatia ni wagombea watafanya midahalo ukianza na Ngome ya Vijana ya vijana utakaofanyika tarehe 27 February na kufatiwa na mdahali wa Ngome ya Wanawake utakaofanyika February 28 na kufatiwa na mdahalo wa watia nia katika nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Chama Mwenyekiti na Makamu wenyeviti utakaofanyika Machi 4 na kubainisha kuwa midahalo yote itafanyika katika ofisi za makao makuu ya Chama Dar es Salaam.
 

No comments