Breaking News

FEMATA YATOA TUZO KWA VIONGOZI WA SERIKALI

Mwanahamisi Msangi na Tito Msellem, Mwanza
Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) limetoa tuzo kwa Viongozi wa Serikali na Vyeti vya Ushiriki kwa kutambua mchango wa wachimbaji wa madini katika hafla ya Usiku wa Madini iliyofanyika tarehe 09 Mei, 2023 katika ukumbi wa Rock City Jijini, Mwanza.

Tuzo zilizotolewa ni pamoja na kwenda kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko kwa kutambua  mchango wao katika usimamizi bora na utekelezaji katika Sekta ya Madini.

Tuzo nyingine ilitolewa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula ya mafanikio bora katika Utendaji wa Tume ya Madini na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba ya Mtendaji bora na mwenye maamuzi pamoja na vyeti vya pongezi kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa nchini kwa usimamizi bora wa sheria, kanuni na taratibu za sekta ya madini katika mikoa wanayoiongoza.

Zoezi hilo la utoaji tuzo na vyeti kwa Viongozi liliendeshwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ambapo aliagiza Wizara na Tume ya Madini kuendelea kuongeza uboreshaji wa kanuni za sheria ya madini pamoja na huduma kwa Wachimbaji Wadogo





No comments