Breaking News

CCM ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI

DAR ES SALAAM
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema  amekutana na kuzungumza na waandishi wa vyombo vya habari (Magazeti, Televisheni, Redio na Blogu) nchini katika kuhakikisha  mahusiano baina ya CCM na wanahabari yanazidi kuwa bora na kuendelea kuimarika, kulingana na mahitaji ya wakati.

Chama Cha Mpainduzi kitaendelea kutambua umuhimu na nafasi ya vyombo vya habari  katika kueneza Sera na Itikadi ya Chama cha Mapinduzi na kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na utendaji kazi wa Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


No comments