Breaking News

SERIKALI INATAMBUA MCHANGO MKUBWA VIONGOZI WA DINI

Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Jumanne Sagini akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini katika mkutano mkuu maalum uliofanyoka katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es salaam.

Viongozi wa taasisi za kidini na mila waakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Jumanne Sagini katika mkutano mkuu maalum uliofanyoka katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Serikali imesema inatambua mchango mkubwa wa taasisi za kidini na mila katika kudumisha misingi ya Amani, Umoja na mshikamano pamoja na mchango unaotolewa na taasisi hizo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu maalum wa jumuia ya maridhiano na amani Tanzania (JMAT), jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Jumanne Sagini amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa jumuia hiyo nchini imekuwa na mchamgo mkubwa hususani katika kuleta Maridhiano.

"Kupitia Mardhiano Mambo mengi  yamekamilika na kuleta Amani, japo kumekuwpo na changamoto tayali serikali imetoa milioni 45 katika kuimarisha utekelezaji wa utatuzi wa changamoto hicho ".Alisema Mhe. Sagini.

Mhe. Sagini pia ametumia nafasi hiyo kuwataka Viongozi wa dini nchini kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na watoto. 

Aliongeza kuwa wizara imekuwa ikifanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya taasisi hizo kwa lengo la kuwezesha uwepo na mazingira bora ya utendaji wa majukumu yao ikiwepo swala la kuwepo na changamoto ya sauti kubwa wakati wa ibada.

"Serikali imekuwa ikipokea mapendekezo na kuyafanyia kazi hususani swala la Sauti kubwa kwenye maeneo ya ibada hususani usiku na tayali tumeanza kuchukua hatua" Alisena mhe. Sagini. 

Aidha mhe Sagini pia amewataka vingozi hao wa kidini kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kuwezesha kuziendesha na kuziimalisha taasisi.

Mkutano huo mkuu wa siku moja umeudhuliwa na vingozi wa dini kutoka mikoa yote nchini.

No comments