Breaking News

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA NGUVU KUFUNDISHA WATAALAM WA DAWA ZA USINGIZI NA GANZI

Dar es Salaam:
Chama cha Wataalam wa Dawa za usingizi na ganzi (SATA) kimeiomba Serikali na wadau kushirikiana kuongeza nguvu kufundisha wataalam wengi zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Chama hicho Dokta Edwin Rwebugisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tatu wa wataalam hao unaofanyika jijini Dar es Salaam.

“Tuombe Serikali na wadau wengine kushirikiana kuongeza nguvu kuweza kufundisha/kutengeneza watoa huduma wengi zaidi na wale waliopo tuendelee kuwaongezea uwezo,” amesema Dkt. Rwebugisa.

Hivyo amesisitiza kwa kusema kwamba juhudi za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha wataalam hao wanaongezeka ili kukidhi mahitaji.

Akizungumza mkutano huo amesema kwamba mkutano huo wa siku tatu unajumuisha wataalam kutoka hospitali zote za kitaifa, mikoa, Wilaya na vituo vya afya kwa wale wanaotoa huduma za usingizi na ganzi.

Kwamba mkutano wa Mwaka huu wanaangalia uboreshaji wa huduma za afya.

“Tupo kwa ajili ya kujifunza namna ya kudhibiti maumivu wakati wa kupewa huduma za afya hususan za upasuaji,” ameeleza.

Kwa upande wake Rais wa Chuo cha Kufundisha Tasnia hiyo katika Nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika, Dokta Mpoki Ulisubisya amesema ametaja Nchi ambazo ziko chini ya Chuo hicho ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokeasia ya Congo (DRC), Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Eswatin, Zambia, Zambia na Lesotho.

Kwamba kwa wapo katika mkakati wa kuongeza wataalam katika Nchi za Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini na Botwasana.

Amesema sababu za kuwepo kwa Chuo hicho ni ili kuongeza nguvu katika kuzalisha wataalam wengi zaidi. 

No comments