Breaking News

DKT. MUCHUNGUZI ATOA USHAURI HUU KWA SERIKALI KUHUSU UTENDAJI MASHIRIKA YA UMMA

Mchambuzi wa Masuala ya Maendeleo, Kikanda na Kimataifa ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AFREDA, Dkt. Dennis Muchunguzi  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyokabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dar es Salaam:
MCHAMBUZI wa Masuala ya Maendeleo, Kikanda na Kimataifa Dkt. Dennis Muchunguzi ameishauri Serikali kufanya maboresho ili kuimarisha utendaji wa mashirika ya umma kwa kupata faida.

Dkt. Muchunguzi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AFREDA ametoa ushauri huo jana jijini Dar es Salaam akizungumzia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyokabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imeonyesha mashirika mengi ya umma kujiendesha kwa hasara.

Miongoni mwa maboresho hayo alieleza kwamba ni kuhakikisha Ofisi ya Msajili wa Hazina inafanya mapitioa upya ya muundo wa mashirika na  malengo ya kuanzishwa kwa mashirika hayo kama yanaendana na wakati wa hivi sasa.

"Tusiangalie tu kwamba mashirika hayapati faida, mashirika haya yalianzishwa miaka mingi sana kwa shughuli mbalimbali, yapo ambayo yanfanya kazi kwa ajili ya kutoa huduma pekee, na yapo ambayo yalianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa faida. Hivyo ni lazima Msajili wa Hazina apitia upya kuona malengo ya kuanzishwa kwa mashirika hayo kama yanaendana na wakati wa sasa," alisema Dkt. Muchunguzi.

Dkt. Muchunguzi aliendelea kueleza kwamba Sheria ya Idadi ya Wajumbe wa Bodi ya Mashirika hayo inatakiwa kuangaliwa upya kwani haiendani na wakati wa sasa kwamba idadi ya Wajumbe wa Bodi inatakiwa kuongezeka kwani yapo mashirika ambayo yana hadi wajumbe watatu jambo ambalo halitoshelezi kuhakikisha ufanisi wa utendaji wa mashirika.

Kadhalika Mchambuzi huyo aliiomba Serikali kuhakikisha Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi wawe wabobezi kitaaluma katika shughuli halisia zinazofanywa na shirika husika, kwamba hili litafanya iwe rahisi kwa wajumbe kufanya kazi katika uwanja ambao wanaufahamu vizuri na hivyo kuchochea ufanisi wa mashirika ya umma na kuepuka hasara.

Dkt. Muchunguzi hakuishia hapo, pia aliiomba Serikali kuhakikisha inawapa mafunzo Wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Umma lengo likiwa ni kuhakikisha wanawekwa sawa kuelewa majukumu yao vyema.

Sambamba na hayo aliitaka Serikali kuipa meno Bodi ya Mashirika ya Umma katika kufanya uamuzi pamoja na kuhakikisha wanaangalia upya muundo wa mashirika hayo.

Akizungumzia Ripoti hiyo ya CAG Dkt. Muchunguzi alisema kwamba pamoja na ripoti kubainisha mapungufu, lakini Serikali inapaswa kupongezwa kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa rasilimali.

*Ripoti ya CAG inamambo makubwa na mazuri ya kupongezwa. Hivyo ni wongeze viongozi wetu Rais Dkt. Samia, Makamu wa Rais Dkt. Mpango, Rais Dkt. Mwinyi, Waziri Mkuu Majaliwa, Bunge na Mahakama kwa usimamizi mzuri. Asilimia 99 ya taasisi zilizokaguliwa zina hati safi na asilimia 4 ni hizo hati nyingine," alisema Dkt. Muchunguzi na Kuongeza,

"Ukusanyaji wa mapato umeongezeka na usimamizi wake ni mzuri. Nipongeze Halmashauri kwani wamefanya usimamizi mzuri. Niipongeze Serikali kwa usimamizi na ukusanyaji mzuri wausimamizwe. Niwaombe Watanzania kuongea mazuri ya ripoti hii na kwa ukubwa hususan  kwenye ukusanyanyi wa mapato na usimamizi wake,".

Akizungumzia kuhusu miko ya asilimia 10 ya halmashauri inayotolewa kwa vijana, kina mama na wenye ulemavu ambayo zaidi ya shilingi bilioni 80 haijarejeshwa alisema huenda tataizo lipo kwenye mfumo wa utoaji wa mikopo hiyo.

Hivyo ameunga mkono ushauri wa Rais Dkt. Samia wa kutaka fedha hizo zipitie Benki na Taasisi za Kifedha (Microfinance Institution).

Hata hivyo ameshauri maofisa wa halmashauri wanaohusika na mikopo wapewe mafunzo ya namna ya kusimamia mikopo hiyo, lakini pia makundi lengwa la vijana, kina mama na walemavu alitaka yapewe mafunzo ya namna ya kutumia mikopo hiyo kwa ufanisi ili kurahisisha urejeshwaji wake.

No comments