Breaking News

ZABRONI SINGERS, JOSHUA NGOMA, CHRISTOPHER MWAHANGILA NA TUMAINI AKILIMALI KUTUMBUIZA TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU..MSAMA AFUNGUKA LITAKUWA LA KIMATAIFA

Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika wakati akitangaza majina ya wasanii watakaoshiriki tamasha la pasala litakalofanyika siku ya 9 April mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa akizungumza juu ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili nchini Christopher Mwahangila akizungmza na waandishi wa habari namna ambavyo amejipanga kuhakikisha akikonga mioyo ya mashabiki siku ya tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika siku ya Aprili 9 mwaka huu katiika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam yanaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habarri jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi pamoja na kutambulisha wasanii watakao tumbuiza siku hiyo amesema tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti na matamasha yote ambayo yamewahi kufanyika hapo awali kwani tamasha la mwaka huu limeboreshwa na litakuwa na viwango vya kimataifa.

“Maandalizi ya Tamasha yanaendelea vizuri na tumejipanga kwa kuwa na Tamasha kubwa na kuweka mkazo zaidi katika ubora ambapo mwaka huu litakuwa ni tamasha lenye viwango vya kimataifa,” Alisema Msama.

Alisema mwaka huu tamasha la Pasaka litakuwa la kipekee kwani ni urejeo mpya kwa kutokana na kutofanyika nchini takribani miaka saba (7) ivyo nitoe rai kwa wapenzi wa tamasha hili kujitokeza kwa wingi kushuhudia jinsi tamasha la mwaka huu likavyokuwa limeboreshwa.

Aidha Msama aliongeza kuwa Tamasha la mwaka huu litafanyika katika viwanja vya Leaders Club hili kutoa nafasi kwa kila mwananchi kufika wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani kuweza kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka katika mazingira mazuri.

Msama aliongeza kuwa Tamasha la Pasaka mwaka huu litaenda sambamba na kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi nzuri ikiwemo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Wote mashahidi katika kipindi cha ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia tumeshuhudia miradi yote ikitekelezwa vizuri na biashara zinaenda vizuri, hivyo tunayo kila sababu ya kumshukuru na kumwombea kwa mwenyezi Mungu kupitia Tamasha hili la Pasaka,” Alisema Msama.

Katika hatua nyinge bw. Msama amewataka wananchi hususan wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hilo kwani usalama upo wa kutosha pamoja na kutapata burudani kutoka wa waimbaji wengi maarufu wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya nchi.

Amewataja Baadhi ya waimbaji ambapo tayali wameshakubali kutumbiza siku ya tamasha hilo kuwa ni Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Tumaini Akilimali kutoka Kenya na Zabroni Singers kutoka Tanzania.

Wengine ni Upendo Ngoma kutoka Tanzania, Masi Masilia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ambwene Mwasongwe kutoka Tanzania na Joshua Mlelwa kutoka Tanzania.

Nae mratibu wa Tamasha hilo bwana Emmanuel Mabisa alisema maandilizi ya tamasha la mwaka huu yanaendelea vizuri na wamejipanga vizuri kwa lengo la kuhakikisha linakuwa na viwango vya kimataifa hususani katika ubora wa jukwaa na suala la muziki.

“Tayali tumeingia makubaliano na kampuni itakayofunga jukwaa la kisasa pamoja na vifaa vya muziki vya kisasa kwaa lengo lankuhakikisha tamasha lawaka huuu linakuwa la viwango vya kimataifa,” Alisema Mabisa

Alisema kwa kuzingatia kuwa tamasha la mwaka huu linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili ya Rais Dkt. Samia hivyo tamasha lawaka huu litakuwa kubwa na la kihistoria nchini.

Kwa upande wake mmoja ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili ambaye atatumbuiza siku ya tamasha hilo, Christopher Mwahangila amethibitisha kushiriki katika tamasha hilo na kuwataka Watanzania kwa ujumla kuhudhuria kwani wamejipanga kutoa burudani nzuri kwani walikuwa wamelimisi Tamasha kwa muda mrefu.

“Mimi ni miongoni mwa waimbaji watakaoshiriki siku ya tamasha la pasaka mwaka huu tulikuwa tumelimisi hili Tamasha notoe rai kwa wananchi hususani wakazo wa mkoa wa dar es salaam na mikoa ya jirani  kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 9 April mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club kwani tamasha la mwaka huu ni bure kabisa,” Alisema Mwimbaji Mwahangila.

No comments