Breaking News

WINPRINCESS BET YAMTANGAZA JOTI NA GIGY MONEY KUWA MABALOZI WAKE

Meneja wa Mchezo wa Kubashiri WinPrincess nchini bwana Hakan Aric akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya kutanganza rasmi mabalozi wa kampuni hiyo iliyofanyika kaika hotel ya New point ( New afrika) jijini Dar es salaam

Dar es Salaam:
Kampuni ya Michezo ya kubashiri nchini Tanzania ya WinPrincess Bet imewatangaza msanii maarufu wa vichekesho Lucas Mhuvile ‘Joti’ na msanii wa musiki wa Bongofleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuwa ubalozi wao.

Akizungumza na hafla ya kuwatambulisha mabalozi hao jijini Dar es Salaam Meneja wa Mchezo wa Kubashiri WinPrincess nchini bwana Hakan Aric, amesema kampuni hiyo kwa kutambua dhamani ya ya wateja wake imeamua kuzingua kampeni mpya ya “Ushindi Papo Hapo” (Immediate Pay-Out”)

“WinPrincess Online Platform inakaribisha watu wazoefu na wapya kubashiri kwenye michezo ya mtandaoni kupitia kampuni hii yenye jumla ya uzoefu wa miaka saba katika kuweka Dau kwenye michezo ya mtandaoni,” Alisema Bw Aric.

Alisema Kubashiri michezo ya mpira na kasino kupitia tovuti ya WinPrincess ina faida nyingi ambazo huleta msisimko wa kweli ikiwemo kuanzia kibashiri na kima cha chini hadi shilingi moja ambayo ni nafuu kwa kila Mtanzania kuanzia miaka 18 na kuendelea, kampuni hii ina odds kubwa kuliko zile zilizopo hapa nchini.

Ameongeza kuwa Ikiwa na lengo la kujali maslahi ya wateja, kuwapa ofa ya asilimia 100 kwa kila mchezaji mpya, uwezo wa kubet mchezo mmoja hadi arobaini, kutoa bonasi kupitia bahati nasibu zetu na bonasi za kurejesha pesa yote haya pamoja na mpango wa uaminifu unaoturuhusu kuwatuza wateja wetu wa kawaida na waaminifu.

Kwa upande wake Meneja Masoko Masoko wa WinPrincess Sports Betting, Bi Winny Macha amesema wao kama WinPrincess tunaamini katika uaminifu na tuko hapa kutoa imani kwa wateja wetu kwa kutangaza kauli mbiu yetu “Ushindi ni Papo Hapo” ambayo ina maana mshindi ana uhakika wa Malipo Papo Hapo kutokana na ushindi wake,

Alisema kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake, tunapenda kuwakaribisha wanachama wapya, hasa wanawake kuja kujaribu jukwaa letu na kujiburudisha kwa hali ya kawaida ya kushinda na kupata zaidi. Odds Bora na Malipo Papo Hapo.
Meneja Masoko Masoko wa WinPrincess Sports Betting, Bi Winny Macha akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya kutanganza rasmi mabalozi wa kampuni hiyo iliyofanyika kaika hotel ya New point ( New afrika) jijini Dar es salaam.


No comments