Breaking News

WAZIRI UWESO KUFUNGA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISAYANSI NA MAJI

Waziri wa Maji Jumaa Aweso anatarajia kufungua Kongamano la Kimataifa la Maji la Kisayansi  litakaloshirikisha Takribani nchi 26 Duniani ambalo litafanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo Cha Maji Dkt Adam Karia wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea kufanyika kwa kongamano hilo ambalo linatarajiwa kuanza siku ya kesho mpaka tarehe Machi,10 Mwaka huu

Amesema katika kongamano hilo kutakuwa na mawasilisho zaidi ya 70 kwa kazi ambazo zimefanyika za utafiti Pamoja na matokeo yake ambayo wameyafanya na hivyo kuleta mafanikio chanya

"Dhumuni letu kubwa ni kuleta uelewa wa pamoja kuhusu kuzijadili changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza katika tasnia ya maji lakini kwani watakuwepo mabingwa wakubwa ambao wataifahamisha Jamii mambo mengi yanayoweza kusaidia kuzitatua changamoto za maji"amesema Dkt Karia

Amesema kuwa wanaliita Kongamano la kimataifa kwa sababu lina sura ya kiduni kutokana na kuwaalika watu kutoka mabara yote Asia,Afrika na hata Ulaya.

Mkuu huyo wa Chuo amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kusababisha Dunia kuwa na changamoto ya maji ni moja ya ajenda ambayo itajadiliwa  katika Mkutano huo.

‘Suala la Mabadiliko ya tabia nchi ndio ambalo limesababisha hali ya maji isiwe kama ambayo tumezoea kuiona lakini pia mambo mengi ya teknolojia yatajadiliwa ili kuhakikisha kwamba vyanzo vya maji vinalindwa’amesema Dkt Karia

Aidha akizungumzia Kongamano la Mwaka Jana amesema lilisaidia Jamii kupata uelewa Mkubwa wa mambo ambayo yalijadiliwa katika Kongamano Hilo.

No comments