Breaking News

WAZIRI AWESO AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI NA MAJI, AKIPONGEZA CHUO CHA MAJI

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Amidu Aweso Akifafanua jambo katika ufunguzi wa kongamano la Kisayansi la Maji linalofanyika katika hotel ya ubungo plaza jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu mkuu wa Wizara Ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea katika kongamano la kimataifa la Kisayansi la Maji linalofanyika katika hotel ya ubungo plaza jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam: 
Waziri wa Maji mheshimiwa Jumaa Awesso amesema serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake wameweza kutatua changamoto ya upakatikanaji wa maji nchini baada ya kuinzisha fedha zilizokwenda kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya maji. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano kubwa la kimataifa liloandaliwa na chuo cha maji lenye lengo kujadili mada mbalimbali pamoja tafiti zenye lengo la kupeana ujuzi juu ya masuala ya maji.

Amesema serikali ya Rais samia imejizatiti kumtua ndoa mama kichwani  baada  ya kipindi cha miaka miwili kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali nchini.

"Kwa kipindi  kifupi cha mama nataka niwahakikishia hakuna mradi wa maji uliosimama miradi yote inaendelea tumeona mradi wa butiama wenye thamani ya bilioni 69" Alisema Mhe.Awesso.

Waziri Aweso ameitaka wizara ya Maji kukitumia wanafanzi na wataalamu wa chuo cha maji maana ni hazina kubwa kutokana na kufundishwa ipasavyo.

Amesewa ni jambo la kushangaza kuona Taifa linatumia wataalamu kutoka nje ya nchi wakati kuna wataalamu wazuri kutoka kwenye chuo cha maji.

Waziri Aweso amesisitiza kuwa atapigania na kuhakikisha kuwa mtaalam kutoka chuo cha maji anakaa mtaani hana kazi na kuelekeza kila mradi wa maji lazima awepo mtaalamu wa masuala ya maji aweze kuendesha. 

Kwa Upande wake, Naibu Katibu mkuu Wizara ya maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema serikali inategemea makubwa kupitia kongamano hilo ambalo litatoa mwelekeo juu ya masuala yote ya maji.

Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa lengo la wizara ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 maji yawe yamepatikana asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini.

Katika kongamano hilo jumla ya mawasilisho zaidi ya 70 za kazi ambazo zimefanyika za utafiti pamoja na matokeo yake ambayo wameyafanya na  kuleta mafanikio chanya zitajadiliwa.

No comments