DIWANI LYOTO ATOA USHAURI KWA SERIKALI KUHUSU SWALA LA USHOGA
Diwani wa Kata ya Mzimuni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Manifredy Lyoto ameishauri serikali kutunga sheria itakayodhibiti vitendo vya ushoga pamoja kuwalinda watoto wadogo hususani walio Kutika shule za bweni.
Lyoto amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa mtamdao huu amesema kuibuka kwa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya ushoga inasababisha kupotea kwa maadili ya kitanzania na kiafrika.
Ni suala ambalo la ajabu hatukudhani kama litatokea lakini mpaka sasa tunavyoongea lipo, hivyo niwaombe viongozi wa dini waongeze bidii kuwafundisha waumini wao kutambua na kujua ubaya wa kitendo cha ushoga kwenye jamii" Alisema
Nakuongeza kwamba Nasisi wenyewe katika jamii yetu mfano mimi kwenye kata yangu nimekua nikiwaita wananchi tunajadili kuhusu masuala ya maadili ya watoto wetu na kama atabainika mtoto anafanya vitendo vya uhalifu ikiwemo ushoga tutamchukulia hatua kali za kisheria.
Aidha amesema kwamba suala hili la ushoga lichkuliwe kwa uzito na kwamba Tanzania kama taifa lazima kuamka nakuhakikisha matendo machafu yanadhibitiwa ili kulinda tamaduni zetu, pia kutumia wataalamu wa vyuo vikuu kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha tatizo hilo nakuchukua hatua.
Hata hivyo amewaomba Wazazi pia kutekeleza wajibu wao wa malezi kwa watoto nakuacha tabia za kupeleka shule za bweni watoto wa shule za msingi kwani kufanya hivo hawapati malezi mazuri na wengine kuanza kufundishwa tabia mbaya ikiwemo vitendo vya ushoga.
Katika hatua nyingine Diwani Lyoto amezungumzia miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwepo madarakani nakusema kuwa uongozi wake umetukuka kwani ameendeleza vizuri miradi mikubwa ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Dkt Jonh Magufuli aliyefariki Dunia mwezi Machi 2021
Amesema kwamba Rais Dkt. Samia ameonyesha ukomavu wake katika uongozi kutokana na kutekeleza miradi mbalimbalj ya Sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu ya Barabara , Maji, Kilimo, Nishati, na kwamba kuwa mwanamke hakumaanishi chochote kuwa hawezi kuongoza.
"Jana amevunja rekodi ya kuhudhuria mkutano wa Baraza la Wanawake la Chama Cha Chadema ( BAWACHA) ameonesha tofauti za kiitikadi, amefanya ambayo wanaume viongozi waliopita hawakufanya, kwasasa hali ya kisiasa imeanza kua tulivu nchini" Alisema Diwani Lyoto.
No comments