Breaking News

MASHIRIKA YA KUTETEA HAKI ZA WASICHANA NCHINI WAITAKA SERIKALI KUWASILISHA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA NDOA NA UMRI WA MSICHANA KUOLEWA

Dar es Salaam:
Mashirika ya kutetea haki za wasichana nchini wameitaka serikali kupitia wizara ya sheria na katiba kuwasilisha muswada Wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 katika bunge lijalo la bajeti  kuwa umri wa miaka 18 kuwa umri wa chini wa kuolewa na kuoa.

Akisoma tamko hilo kwa niaba ya mashrika 58 jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative Bi. Rebeca Gyumi amesema takribani miaka 4 sasa serikali kupitia muhimili wa bunge na wizara ya sheria na katina imekuwa ikishindwa kutekeleza kwa wakati na kuchukua hatua stahiki na za haraka kuifanyia maboresho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

"Takribani miaka minne sasa serikali kupitia muhimili wa bunge na wizara ya katiba wamekuwa wakishindwa kutekeleza na kuchukua hatua stahiki za haraka kuifanyia marekebisho ya sheria za ndoa ya mwaka 1971 kifungu namba 13 na 17 kama ilivyoamriwa na mahakama ya rufani" Alisema Bi Gyum.

Alisema mashirika ya haki za wasichana nchini tunatoa wito kwa serikali kujielekeza katika hukumu iliyotolewa na mahakama ya rufani kuhusu umri wa kuolewa kwa kuwasilisha muswada wa mabadiliko sheria hiyo katika bunge la bajeti kuweka umri wa miaka 18 kuwa umri wa chini wa kuoa na kuolewa kwa wasichana na wavulana.

Aidha Bi Gyum amewakumbusha wabunge kutambua kuwa ni wajibu wao kuwalinda watoto na ndoa za utotoni  bila kujali wapo shule au nje ya shule kwani ni bado watoto na wanatakiwa kuwekewa mifumo ya kuwalinda na kuwekeza zaidi katika ustawi wao.

Alisema kupitia tamko hili mashirika hayo yameazimia na kuona kuwa swala hili linahitaji sauti za makundi yote hasa wapenda haki ja ustawi wa mtoto wa kike hivyo kahamasisha wananchi kudai uwajibikaji kwa wabunge wa bunge la jamhuri yauumgano wa tanzania kufanyia mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 katika vifungu vya 13 na 17.

Bi Gyum aliongeza kuwa kupitia tamko hili tumekubaliana kuwa hakuna maendeleo tatakayoweza kuyafikia kama nchi  bila kutokomeza bdoa za utotoni kwani ndoa hizo zimekuwa zikiathiri wasichana wengi hasa wa tabaka la chini ambao wengi wao wanatokea familia maskini hivyo kitendo cha kuendelea kuwa na sheria inayoamashisha ndoa za utotoni ni kuendelea kuongeza umaskini katika taifa na kuwanyima wasichana hasa wanaotoka katika familia maskini au vijijini haki yao ya msingi ya kulindwa utu wao na kufuraia utoto wao

No comments