Breaking News

MANDONGA BALOZI MPYA WA NYUMBA FASTA, AJA NA NGUMI YAKE MPYA

Bondia maarufu nchini Karim Mandonga Akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa balozi wa nyumba fasta. 

Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi maarufu Tanzania Karimu Mandonga (Mtu kazi) Leo tarehe 17 March 2023 amepata dili ya ubalozi kutoka kampuni ya Nyumba Fasta, Tukio lilofanyika katika ofisi za Nyumba Fasta kijitonyama Victoria Jijini Dar es salaam.

Karim Mandonga ambaye amekuwa akipata dili mfululizo za ubalozi kutoka a mbwembwe na umaarufu wake katika mchezo wa masumbwi, Nayo kampuni ya Nyumba Fasta wameweza kumpa ubalozi kwa ana vigezo vyote vya kufanya kazi na Kampuni ya Nyumba Fasta ambao ametambulisha mfumo mpya wa kidigital. 

Waandishi wa habari wameweza kumuuliza Karim Mandonga siri ya mafanikio yake ya kupata dili za ubalozi mfululizo ikiwemo hili dili kubwa la ubalozi wa kampuni ya Nyumba Fasta

Mandonga akijibu swali hilo amesema "Wakati wa Mungu ni wakati sahihi, Mwenyenzimungu Ana uwezo wake, hivyo kapewa ubalozi wa nyumba fasta ni uwezo wa Mungu" 

Pia karimu Mandonga ametambulisha ngumi yake mpya inaitwa Mlungambunga ambayo imetokana Jangwa la sahara inayompoteza mtu hewani. 

Naye Meneja masoko kampuni ya Nyumba Fasta Robbison Marley amesema mfumo wa nyumba fasta ni mfumo wezeshi ambao utawasaidia watu wa chini na wa kawaida ambao wanaotaka nyumba nzuri na kiurahisi, mfumo huu hauna malipo ya dalali kwani kupitia simu yako ya mkononi utakuwezesha kupata nyumba nzuri kwa muda Muafaka. 

Nyumbafasta ni mfumo wa kidijitali unaokuwezesha kupata nyumba za kupanga bila malipo ya kodi ya  mwezi mmoja na kupata mawasiliano ya mwenye nyumba mojakwamoja kwa gharama ndogo kuanzia shilingi elfu moja vilevile nyumba fasta inakuwezesha kununua au kuuza nyumba au ardhi zilizohakikiwa wauzaji ili kujiepusha na migogoro. 

Nyumba fasta imetengenezwa na vijana wa kitanzania na inapatikana mtandaoni Tanzania nzima kupitia tovuti ya  www.nyumbafasta.co.tz kwa kutumia simu janja(smartphone) mwenyenyumba anaweza kusajili nyumba yake na mpangaji anaweza kutafuta nyumba ya kupanga kokote pale Tanzania.

Kupitia nyumba fasta mpangaji anaweza kupata nyumba yenye ubora kwa gharama nafuu, Mfumo huu ni rahisi kuutumia kwa kuwa umetengenezwa na vijana waandisi wazawa wanaojua watanzania wanahitaji nini, Mfumo huu unasaidia kuokoa muda ambao mpangaji anautumia kupata nyumba vilevile mfumo huu unasaidia kuepusha migogoro isiyo ya lazima wakati wa kununua nyumba au ardhi.

Nyumba fasta inakitengo cha huduma kwa wateja kinachotoa huduma bora na kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa wakati.

Nyumbafasta inatoa wito kwa wenyenyumba za kupanga Tanzania nzima kujisajili kupitia tovuti yetu www.nyumbafasta.co.tz na kupitia mawakala wetu wa nyumbafasta watakao kuwa wakifanya kampeni ya usajii ya mtaa kwa mtaa kwanzia mkoa wa Dar es Salaam.

Tunawakaribisha kutumia nyumba fasta kwenye huduma ya ununuzi na upangaji wa nyumba bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja.

MALIPO YA KODI YA MWEZI MMOJA
Panga, pangisha Nyumba  kidigitali na NYUMBAFASTA

No comments