Breaking News

DAR ES SALAAM QUALTY MOTORS YAMTANGAZA MZEE MPILI KUWA BALOZI WAKE

Afisa masoko wa kampuni hiyo Bi. Shemsa Saidi Msellem akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya kumtangaza balozi wao mpya Mzee Mpili. Iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam
Balozi wa mteule wa kampuni ya Dar es salaam Quality motors, Mzee Mpili akifafanua jambo kwa waandiahi wa habari katika hafla ya kutangazwa rasmi kuwa balozo wa kampuni iliyofanyika jijini Da es salaam.

Sehemu ya vifaa mbalimbali vinavyouzwa na kusambazwa na kampuni ya Dar es salaam Quality motors,
 

Dar es salaam Quality motors inayo jishunghulisha na uuzaji na kusambaza spea mablimbali za magari leo imemtangaza mzee mpili kuwa balozi wake mpya wa kampuni hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza balozi huyo iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam Afisa masoko wa kampuni hiyo Bi. Shemsa Saidi Msellem Amesema kampuni hiyo kwa kutambua ushawishi alionao mzee mpili imeamua kufanya nae kazi kwa lengo la kuhakikisha wanawafikia wateja wake kote nchini.

"Sisi Dar es salaam Quality motors leo tunapenda kumtangaza balozi wetu mpya ambaye atatangaza bidhaa zetu bihaa ambazo zina ubora wa viwango vya kimataifa kwa ajili ya magari ya aina mbalimbali" Alisema Bi. Msellem

Aidha bi aliongeza kuwa wao kama wauzaji wa spea madhubuti za magari wameona firsa kupitia mzee mpili kuweza kufikia wateja wao nchi nzima kwani bidhaa tunazouza zote zina viwango vya hali ya juu vya ubora pamoja na kukidhi hali ya barabara zetu.

Kwa upande wake balozi wa Dar es salaam Quality motors, mzee mpili alisema nianze kuwashukuru kwa kutambua na kudhamini kazi yangu mpaka kumteua kuwa balozi wenu.

"Natambua kama kampuni mlikaa  na kutambua mchango wangu hasa kupitia kazi nazofanya na kuona nafaa kuwa balozi wenu napenda kuwahaidi kuwa kupitia ubalozi huu sitawaangusha" Alisema Mzee Mpili.

Aidha pua mzee mpili leo ametangaza rasmi kuwa ameanza kutangaza ambopo atakuwa kaitangaza kupitia atelevision ya mtandaoni ya Swahili media ambapo amewataka wadau kufatilia kipindi chake kuona namna ambavyo amejipa.

Amekitaja kipindi icho kuwa ni Miyeyusho ya Mzee Mpili ambacho kitakuwa kinatoka kupita televisheni ya mtandaoni ya swahili media.

No comments