Breaking News

TMA YASITITIZA UMUHIMU WA KUFIKISHA TAARIFA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA UHAKIKA, USAHIHI NA KWA WAKATI

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesisitiza umuhimu wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutolewa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi. 

Haya yalizingumzwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a wakati akifungua Warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2023 yenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa maendeleo endelevu”.
 
“Kama mnavyofahamu warsha hii ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati. Napenda kuendelea kuwashukuru wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii (Online Media) kwa kuendelea kuwa nguzo muhimu katika kusambaza na kufikisha taarifa za hali ya hewa pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji yaani jamii kwa ujumla Hii imesaidia katika kuongeza uelewa na mwamko wa jamii katika kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa”. Alisema Dkt. Chang’a.
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatarajia kutoa rasmi taarifa ya msimu wa mvua za Masika, Tarehe 22 Februabri 2023, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

 

No comments