MSAMA ATANGAZA LIST YA WAIMBAJI NYIMBO ZA INJILI WATAKAO PANDA JUKWAANI SIKU YA TAMASHA LA PASAKA 2023
Mkurugenzi wa Msama Promotion bwana Alex Msama ametangaza list waimbaji wa nyimbo za injili na kuabudu waliothibitisha kushiriki katika tamasha la pasaka litakalofanyika Aprili 9, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya kutangaza majina ya wasanii hao amewataja waimbaji hao kuwa ni Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Tumaini Akilimali kutoka Kenya na Zabroni Singers kutoka Tanzania.
Wengine ni Upendo Ngoma kutoka Tanzania, Upendo Nkone kutoka Tanzania, Masi Masilia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ambwene Mwasongwe kutoka Tanzania na Joshua Mlelwa kutoka Tanzania.
“Kwasasa tunafanya mazungumzo na waimbaji kutoka Afrika Kusini, Uingereza na Marekani,” amesema Msama.
Msama ameeleza kuwa Tamasha hilo litakuwa zuri na kubwa la kimataifa na la kihistoria ikizingatiwa halijafanyika kwa takribani miaka saba iliyopita.
Amesema tamasha hilo litakuwa na waimbaji wengi, nguli, wakubwa na wakihistoria, hivyo amewataka Watanzania kujiandaa na tamasha hilo.
Aidha Msama ameeleza kuwa watatumia tamasha hilo kueleza mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka miwili ya utawala wake.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha la pasaka mwaka 2023 bwana Emmanuel Mabisa alisema mwaka huu wamejipanga vizuri na wataakikisha kuwa tamasha la mwaka huu linakuwa bora zaidi ukilinganisha na yaliopita
“Tamasha la pasaka la mwaka huu tumejipanga liwe la hadhi ya kimataifa tofauti na miaka iliyopita hasa katika viwango vya mziki na jukwaa na tayali tumeshapata kampuni itakayofunga vifaa vya muziki vya kisasa,” alisema bw. Mabisa.
Aidha bwana mabisa aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu kuyokana na kutokana na kutokushanyika kwa kipindi kirefu nchiki kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo janga la UVICO 19 tumejipanga mwaka huu kuhakikisha tunatafanya tamasha kubwa na la kihistoria sambamba na kusherehekea miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia.
No comments