Breaking News

MANDONGA AJITOSA KATIKA MUZIKI, KUONEKANA KATIKA VIDEO YA “UMEYAKANYAGA"

Msanii  wa Muziki wa Singeli Chudy Love leo Ijumaa ya Februari 17, 2023 ametangaza rasmi kuzindua video ya wimbo wake mpya unaojulikana kama “Umeyakanyaka”,  ambapo video ya wimbo huo ameshiriki Bondia maarufu nchini Karimu Mandonga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam msanii Chudy Love amesema hafla ya uzinduzi wa wimbo huo utaenda sambamba na shoo kabambe itakayofanyika katika ukumbi wa kisasa wa Small Planet kuanzia majira ya saa 2 usiku.
 
Alisema kwa dhati anamshukuru Mandonga kwa kutaambua kipaji chake na kukubali kuunga mkono muziki wake hiyo ni kutokana na kuona na kutambua kipaji kilicho ndani yake na kuamua kumsapoti katika harakati zake.

“Namshukuru Mandonga kwa kunisapoti katika muziki wangu, kipo kitu amekiona kwangu na kunitangaza, twendeni YouTube tukauone wimbo huo na niwakaribishe baadaye hapa Small Planet,” Alisema msanii Chudy Love.

Kwa upande wake bondia Mandonga alianza kwa kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Umeme Bei Poa bwana G Maker kwa kumsapoti msanii huyo.

Amesema atatoa sapoti kubwa kwenye shoo ya Chudy Love ambayo itaambatana na utambulisho wa video mpya ya wimbo wa “Umeyakanyaga”.

“Anayemdiss huyu msanii kwa wimbo wake wa Umeyakanyaga hatuangalii, sisi tunachosema ni wakati wa Mungu ndio sahihi,” Alisema Mandonga.

Mapema Mkurugenzi wa kampunj ya Umeme Bei Poa ambaye pia ni Meneja wa Msanii huyo, bwana G Maker ameeleza kufurahishwa na uwepo wa Mandonga katika utambulisho wa wimbo huo.

“Mandoga ameingia kwenye muziki kwenye wimbo unaojulikana kama Umeyakanyaga, na leo kutakuwa na usiku wa Umeyakanyaga,” Alisema Bw. G Maker.

No comments