Breaking News

KMC YAPOKEA BUS LA KISASA KUTOKA NBC

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makala kionyesha mfano waufunguo katika hafla ya makabidhiano ya bus kati benki ya NBC na Timu ya KMC yaliofanyika yaliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa masoko kutoka kampuni ya Africarries Ltd, Bwana Zain Pirbhai akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla ya kukabidhiwa bus hilo iliyofanyika jijini Dar es salaam. Alisema Bw. Pirbhai.
Bus ambalo wamekadhiwa timu ya KMC na benki ya NBC
 

Dar es salaam:
Timu ya KMC inayoshiriki ligi kuu ya NBC Tanzania imepokea mkopo wa bus kutoka Bank ya NBC, Tukio la makabidhiano limefanyika leo katika ofisi za Bank makao makuu zilizopo Posta Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika Hafla Hiyo mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema anawashukuru Bank ya NBC kwanza kwa kudhamini ligi yetu pendwa na pia ameamua kuwasaidia KMC kwa kuwapa mkopo wa Bus la Kisasa kabisa.

"Nitoe pongezi za dhati kabisa kwa benki ya NBC kwa kudhaamini ligi kiu na sasa kuendelea kuboresha ligi hiyo kwa kutoa mikopo kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo jambo hili limeifanya ligi yetu kutajwa kuwa moja ya ligi bora ukanda wa afuka mashariki na barani afrika kwa ujumla" Alisema Mhe. Maakala.

Alisema bus hilo ni la mkopo viongozi wa timu na watambue kuwa dawa ya deni ni kulipa hivyo nitoe rai kwa vioungozi wa timu kulipa mkopo kwa wakati na kuwasihihi viongozi hao kulitunza bus hilo hili liweze kufikia malengo ya kununuliwa.

Kwa upande wake Meya wa kinondoni, mheshimiwa  Songolo Mnyonge amesema watahakikishia kuwa mkopo waliopata watalipa kwa wakati kwani NBC wamesaidia kutatua tatizo la usafiri Hivyo hawana budi kuwalipa kwa wakati ili hizo pesa zikawasaidie wengine wenye uhitaji.

Nae mwakilishi wa kampuni ya Africarries Mkurugenzi wa masoko kutoka Africarries Zain Pirbhai amesema wamedhamiria kuboresha ligi kuu ya Tanzania kwa kutengeneza mabasi Kisasa kuendana na thamani ya ligi kuu ya NBC Tanzania

"Tumedhamiria kuboresha ligi ya NBC Tanzania kwa kutengeneza na kuuza mabasi ya Kisasa kuendana na thamani na bora wa ligi, Hivyo mashabiki wategemee Timu zinginezo zinazoshiriki ligi kuu kupokea mabasi yenye ubora kutoka Africarries" 

No comments