KITENGE ATANGAZWA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA VIJANA REAL ESTATE, WAJA NA MRADI MKUBWA WA VIWANJA
Kampuni ya Vijana Real Estate imempa Ubalozi wa kutangaza viwanja vyao vilivyopo Kilomo Bagamoyo mkoani Pwani mtangazaji wa Maulid Kitenge ikilenga kufikisha taarifa hiyo kwa wananchi waliowengi ili wawe nao wamiliki wa viwanja.
Akizungumza katika hafla ya kumtangaza balozi wake mpya jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo bwana Azaidu Daudi Mohamedi amesema mradi huo hadi kukamilika umechukua takribani mwaka mmoja ili kuhakikisha kuwa wanawapatia watanzania viwanja vilivyo bora na vya uhakika vikiwa vimekamilika na hati zake.
“Kampuni yetu ina miaka mitatu tangu ianzishwe na tumekuwa tukiuza viwanja maeneo tofauti nchini ikiwemo Bunju, Mbezi Mpigi Majohe, Madale na Mbweni na kwa sasa tunavyo viwanja Kilomo na mradi huu umechukua takribani mwaka mmoja ambapo tulikuwa tunahakiki maeneo hayo kwa kuyapima na atakayenunua atakabidhiwa hati yake” Alisema Bw. Daudi.
Alisema viwanja hivyo vina ukubwa tofauti kuanzia Square mita 450 hadi 1000 na bei inaanzia milioni 4 na kuendelea na pia unaweza kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi 6 na ukikamilisha malipo unakabidhiwa hati yako.
Aliongeza kusema kuwa lengo lao ni kutaka kila mmoja amiliki kiwanja hivyo watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani viwanja hivyo vipo sehemu nzuri ambayo huduma zote muhimu zinapatikana.
Kwa upande wake Balozi wa kampuni ya Real Estate Mradi wa Kilomo Bagamoyo Maulid Kitenge amewataka Watanzania kuchangamkia fursa hiyo ya viwanja ambavyo ni vya uhakika na vipo sehemu nzuri wanaweza kujenga nyumba za aina tofauti tofauti na kupata huduma zote muhimu.
Aidha amesema mradi huo wa Kilomo upo Bagamoyo umbali wa kilomita 4 kutoka barabara kubwa na komita 8 kutoka eneo la ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Bagamoyo.
“Hakuna baba mwenye gari baba ni mwenye nyumba na katika mradi huu tayari maeneo hayo yamechangamka kibiashara na mimi nilienda mwenyewe nikajiridhisha kuwa umbali huo ni sahihi niwashukuru sana vijana real estate kwa mradi huu na uwekezaji ni kuwekeza kwenye ardhi” Alisema Balozi Kitenge.
No comments