Breaking News

JICA WAFANYA KONGAMANO LA KIHISTORIA LA UBUNIFU BAINA YA JAPAN NA TANZANIA, VYUO VIKUU VYATAKIWA KUJA NA PROGRAM ZA TEHEMA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza katika ufunguzi wa  Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9, 2023 katika ukumbi wa maktaba mpya Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akipokea vitabu mbalimbali  vilivyoandikwa na Wajapan, kwa ajili ya  Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9, 2023 katika ukumbi wa maktaba mpya Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkuu wa Ofisi ya JICA Tanzania,  Yamamura Naofumi akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9, 2023 katika ukumbi wa maktaba mpya Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taaluma Profesa Bonaventure Rutinwa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9, 2023 katika ukumbi wa maktaba mpya Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.

Dar es salam:
Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu ya juu nchini zimetakiwa kubuni programu za TEHAMA ambazo zinazoendana na mwendelezo mzuri wa maendeleo yanayotokea Duniani kote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dokta Francis Michael wakati akifungua kongano la siku mbili la ubunifu baina ya Japan na Tanzani lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu ch Dar es Salaam (UDSM).

“Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu ya juu nchini lazima vije na programu za TEHAMA zinazoendana na maendeleo TEHAMA Duniani, vinginevyo Vyuo vitakuwa vikitoa wahitimu ambao wapo nyuma katika maendeleo ya Teknolojia  na hivyo kushindwa katika ushindani wa soko la ajira duniani,” Alisema Dkt. Michael.

Alisema kongamano hilo ni sehemu ya maadhisho ya miaka 60 ya JICA tangu kuanza shughuli zake nchini sambamba na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kuandhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa.

Vile amesema ni sehemu ya mwendelezo wa mashirikiano yaliyopo baina Japan na Tanzania.

“Lakini siku ya leo ni siku mahususi ambayo Ubalozi wa Japan kupitia JICA wamekutana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwanza kufanya kongamano na majadiliano yanayohusu mustakabali mzima wa ubunifu na maendeleo endelevu ya nchi hizi mbili,” Alisema Dkt. Michael na kuongeza,

“Kwahiyo kimsingi, ni siku ambayo kuna mjadala wa ubunifu kwa ajili ya maendeo ya nchi zote mbili kupitia JICA,”.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taaluma Profesa Bonaventure Rutinwa amesema lengo la kongamano hilo ni sehemu ya uanzishwaji wa programu ya mafunzo yatakayowezesha Tanzania kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza kwanza kutoka nchi ya Japan.

“Japan ina sifa ya peke yake ni nchi iliyoendelea katika viwango vya juu vya maendeleo bila kuiga na kufuata mbinu walizotumia watu wa Magharibi. Na vile vile wameweza kuendelea bila kupoteza utamaduni wao,”Alisema Prof. Rutinwa na kuongeza kuwa,

“Sisi Tanzania tungependa kufikia maendeleo yetu bila kupoteza utamaduni wetu na mazingira yetu, tunaweza kujifunza pale,”.

Prof. Rutunwa amesema kwamba Japan ni nchi ambayo imepiga hatua kubwa sana ya teknolojia hususani kwenye matumizi ya zana za umeme (industrial revolution,”.

Naye Mwakilishi Mkuu wa Ofisi ya JICA Tanzania,  Yamamura Naofumi amesema mwaka 2018 JICA ilianzisha programu ya masomo ya maendeleo kwa lengo la la kuandaa viongozi wajao katika nchi zinazoendelea.

“Programu ambayo iliitwa ‘JICA program for Japanese Studies ambayo inatoa fursa ya masomo kwa Vyuo vya Japan kwa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea kama Tanzania kwa ajii ya kijifunza na kupata ujuzi na historia ya kipekee na utamaduni wa Japan,”.

Hivyo amesema leo na kesho kutakuwa na fursa ya kujifunza na kupata uzoefu wa moja ya shughuli ya program ya  JICA juu ya masomo ya Japan kupitia majadiliano kwenye mada ya ubunifu “Inovation for national growth and sustainable development”.

Amesema ni matumaini yake kwamba siku hizi mbili zitaisaidia sana Tanzania kipiga hatua zaidi kupitua ubunifu kwa kubadilishana maarifa na uzoefu kutoka nchi zote mbini za Japan na Tanzania.

Matukio katika picha mbalimbali ya washiriki wa ufunguzi wa kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9, 2023 katika ukumbi wa maktaba mpya Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.



No comments