Breaking News

WAFANYABIASHARA WA SINZA KWA REMMY WAITAKA SERIKALI KUINGILIA KATI SAKATA KUVUNJIWA VIBANDA VYAO KUPISHA UWEKEZAJI

Wafanyabiasharq wanaofanya biashara zao katika eneo la Sinza kwa Remmy jirani na kwa Kibaden Sinza B wameiomba Serikali ngazi za juu kuingilia kati sakata hilo.

Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao Aswile Adamson amesema kwamba kabla ya kuhamishwa wangetakiwa kutengenezewa mazingira ya mahali pengine pakuhamia kwani kupitia biashara zao wanasomesha na kulipa kodi.

“Je tunaenda wapi, basi wangetutengenezea mazingira ya mahali pa kwenda kwani tunasomesha na kutoa kodi,” amesema Adamson na kuongeza,

Alisema Tunaiomba Serikali itusaidie ngazi ya chini tunapata shida sana, Serikali itusaidie wananchi wake tunanyanyasika na hatujui hatma yetu

Amesema ikiwa kama wanataka kutuondoa sie hatuna tatizo ila tunataka wafuate taratibu za kisheria.

Kwa upande wake Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Shina namba nane katika eneo hilo Bi. Maua Ramadhan akizungumzia mgogoro wa eneo hilo alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo ni kuwa eneo hilo linataka kufanywa Garden (Bustani).

Hata hivyo amedai kwamba tangu mgogoro huo uanze hakuwahi kushirikishwa, lakini alishirikishwa siku wanataka kuweka kibao japo pia hakuhudhuria siku hiyo kwa sababu hakishirikishwa tangu mwanzo.

Amebainisha kwamba wafanyabiashara hao wapo muda mrefu tangu yeye ni msichana mdogo kwani walioanzisha wameshaondoka na wapo wengine.

Ameeleza kwamba kinachoonekana ni kuwa wanaotaka kuwaondoa hawajafuata utaratibu.

Mapema akizungunza na wafanyabiashara hao Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi Urafiki, Bwana Frank Nkusa amewasihii na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu wakati jambo lao linatafutiwa ufumbuzi.

Amesema jambo hilo litapelekwa kwa afisa mipango miji kwani lengo la kupata ufumbuzi wa mgogoro huo jambo litakalosaidia umalizike kwa amani na mambo mengine yaendelee.


No comments