AGA KHAN NA ELEKTA WASAINI MKATABA MANUNUA NA UWEKAJI WA VIFAA VYA KISASA VYA TIBA YA MIONZI
Taasisi ya utoaji wa huduma za afya ya Aga Khan Tanzania na Elekta wametiliana saini mkataba wa manunuzi wa vifaa tiba vya mionzi vitakavyofungwa katika kituo cha utoaji wa huduma za saratani jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla ya utiaji wa saini iliyofanyika jijini Dar es salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Saratani na meneja mtambuka wa wa saratani Tanzania (TCCP), Dokta Harrison Chuwa amesema teknolojia hiyo itasaidia wagonjwa katika utoaji wa huduma bora nchini na ukanda wa afrika mashariki.
"Teknolojia hii ambayo itatumika ni yabkwanza nchini na ya pili katika ukanda wa afrika ya mashariki na kati itasaidia katika hutoaji wa huduma bora za afya nchini na katika ukanda huu wa afrika ya mashariki kwani ni moja ya Teknolojia bora zaidi ya matibabu ya saratani" Alisema Dkt. Chuwa.
Alisema vitaa hivyo viwili vitakavyo fungwa ni model za linear accelerator cha kuongeza kasi ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi na Teknolojia ya Versa HD kutoka elekta yenye mifumo ya Hexa POD na teknolojia ya kisasa ya multi leaf cllimator ambayo uruhusu aima zote za matibabu kupitia tiba ya mionzi 3D, CRT, VMA na IMRT.
Dkt Chuwa aliongeza kuwa mkatana huu wa manunuzi na uwekaji wa mashine za mionzi unakifanya kituo cha matibabu ya saratani kuwa na mashine za kisasa ya kwanza ya aina yake nchini na kwa kanda ya afrika ya mashariki.
Kwa upande wa wake mkurugenzi wa tiba na afya, mtandao wa maendeleo wa Aga khan (AKDN), Dokta Gijs Walvaren amesema lengo kubwa ni kukuza ubora na utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa na kuongesa kwa upatikanaji wa huduma ya msingi hadi ngazi ya tatu.
"Leo kubwa la taasisi yetu ni kuhakikisha kuwa tunakuza ubora wa utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa sambamba na kuongeza upatikanaji wa huduma za msingi hadi ngazi ya tatu kupitia uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikijumuisha vifaa, teknolojia, uwekezaji wa wafanyakazi wenye uwezo pamoja na ithibati ya JCI hivyo kufanya kituo cha saratani cha Aga khan kuwa moja ya vituo bora ulimwenguni." Alisema Dkt. Walvaren
No comments