Breaking News

ACT WAZALENDO WATOA USHAURI KWA SERIKALI NAMNA YA KUKABILIANA NA KUKUA KWA DENI LA TAIFA

Chama cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali kuja na mpango na mkakati maalum ambao utasaidia kumaliza au kupunguza kwa kiasi kikubwa deni la ndani ambalo limekuwa kwa asilimia 30 ambapo athari zake zinakwenda moja kwa moja kwa wananchi.

Akizungumza Makao.makuu ya chama hicho jijinj Dar es salaam, msemaji wa sekta fedha (Waziri wa Fedha na Mipango) wa Chama cha hicho bwana Emmanuel Mvula amesema kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo inaonesha kuwa kumekuwepo na ongezeko la kasi na kukua kwa kiwango kikubwa cha deni la Taifa likiwemo deni la ndani.

Amesema deni la ndani ni hatari ikizingatiwa kuwa limeongezeka kutoka Trillion 18.6 hadi 26.6, ni fedha nyingi huku akifafanua deni la ndani linatokana na Serikali kukopa kukopa benki za ndani, mifuko ya hifadhi ya jamiii, bima na watu binafsi kwa kupatia hatifungani.

"Kwa mujibu wa ripoti Serikali imekopa asilimia 27 ya deni la ndani ambapo asilimia 28 ya deni hilo imekopwa kutoka Taasisi za fedha, asilimia 18 zinatoka bima na asilimia nyingine kwa watu binafsi. Kwa kipindi cha miaka 20 kumekuwa na ukuaji wa hili deni ambapo Mwaka 2005 deni la nje lilikuwa dola bilioni 8 sawa na trilioni 9 wakati deni la ndani lilikuwa Sh.Trilioni 1.7" alisema Bw.Mvula na kuongeza kuwa

"Mwaka 2015 wakati Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa dola bilioni 15.4 wakati deni la ndani likiwa Sh.trilioni 7.9. Hiyo ilikuwa miaka 10 ya Kikwete na alipoingia Rais Dk. John Magufuli hadi kufika Machi deni la nje lilikuwa dola bilioni 24 na deni la ndani Trilioni 16.1. Wakati wa Rais Samia Suluhu Hassan naingia hadi kufikia Novemba mwaka 2022 deni la nje limefikia Dola bilioni 27.5 na deni la ndani Sh.trilioni 26,".

Alisema kukua kwa deni la Taifa hasa deni la ndani kuna athari kubwa amzitaja athari hizo kuwa ni pamoja na kwenda kwa moja kwa moja kwa wananchi huku akieleza deni la ndani halitakiwi kuzidi asilimia 20 na kama nchi tuko asilimia 30 ambayo ni asilimia 10 zaidi hivyo kuongeza Athari nyingine ambayo ni kutumia fedha nyingi kulipa deni.

Bw Mvula aliongeza kuwa makusanyo yetu ya ndani yanatumika kulipa deni ambapo tunatumia bilioni 900 kwa mwezi kulipa deni la Taifa. Kila mwezi tunalipa kati ya bilioni 600 zinatumika kulipa deni la ndani na bilioni 300 zinalipa deni la nje jambo linalopelekea Serikali kutumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko kufanya maendeleo.

Bwana Mvula alibainisha kuwa madeni haya yanatokana na Serikali kukopa katika taasisi za ndani, watu binafsi na kampuni za bima deni linapotakiwa kulipwa Serikali inabidi iingie tena kukopa fedha kwa ajili ya kulipa, hivyo Serikali inakopa zaidi na inaingia kwenye soko la ndani kukopa na inapokopa inaleta ushindani.

Amessema ili kupata fedha za kulipa deni ndio unaona kumekuwepo na utitiri wa kodi,athari nyingine ni kwenda kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya mifuko ya jamii na hivyo inakwenda kuathiri mifuko hiyo na wastaafu kutolipwa pensheni zao kwa wakati.

Madeni hayo yanasababisha mzigo mkubwa kwa wananchi. Kutokana na maelezo hayo ACT Wazalendo tunatoa pendekezo ili kuondoa deni

Alisema Serikali ije na mkakati maalum wa kumaliza deni hilo kwenye bajeti ya mwaka huu na kwa kuwa tunakwenda kwenye maandalizi ya bajeti basi tunaitaka Serikali ije na mkakati wa kumaliza deni.

No comments