Breaking News

WANANCHI TUMIENI UTALII WA UTAMADUNI KAMA NJIA YA KUWAVUTIA WAGENI

WANANCHI wametakiwa kutumia Utalii wa Utamaduni kama njia mojawapo ya kuwavutia wageni wanapokuja nchini ili waweze kuvutiwa na aina mbalimbali za utalii watakaoukuta.

Kaimu Kamishna wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Saadani, Ephahem Mwangomi aliwaeleza wageni kutoka Taasisi inayojihusisha na Utalii wa Kiswahili na Utamaduni (SUUKI)  walipotembelea hifadhi ya Saadan ambapo amesema kuna hazina kubwa ya Utalii wa Utamaduni ambao ikitumika vema inaweza kuwa fursa ya kuendeleza Utamaduni hapa nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi wa SUUKI Joseph Andrew amesema malengo yao ni kutoa elimu kwenye shule na baadae kuwapeleka wanafunzi kwenye vivutio vya utalii. 
Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya Utalii wa Royal Tour ikiwa ni mahsusi kwa nchi ili kuwavutia wawekezaji wa utalii na watalii kuja kujionea Utamaduni halisi wa kitanzania.

No comments