Breaking News

NASS SPORT SOLUTION YAZINDUA SHINDANO LA AFTER SCHOOL CLASH

Kampuni ya Nass Sports Solution ambayo inainua Vipaji vya michezo kwa vijana imezindua rasmi shindano la mpira wa miguu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na sita yanayoitwa After Shool Clash kwa lengo la kuwaunganisha vijana hao wakati wakisubiri kujiunga kidato cha tano na vyuo.

Akizungumza wakati wa halfla ya ufunguzi iliyofanyika katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Nassoro Mungaya amesema jumla ya timu 8 zimejisajiri kushiriki mashindano hayo ambapo zawadi mbalimbali zinatarajiwa kutolewa washindi.

Amesema shule zitakazo shiriki mashindano hayo zimegawanywa katika makundi A na B yenye timu 4 kila kundi, ambapo mshindi wa kwanza anatarajiwa kupata kombe na medali wakati mshindi wa pili na watatu watapata Medali.
Amezitaja zawadi nyingine kuwa ni mfungaji bora, mchezaji bora pamoja na golikipa bora, ambapo amewaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuunga mkono mashindano hayo kwa kufadhili kwani mashindano hayo yanamelenga la kuibua vipaji vya vijana.

"Tuna jumla ya timu 8 zitakazo zitachuana vikali kutoka katika shule mbalimbali hili kumpata mshindi na lengo kubwa ni kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao pamoja na kuwakutanisha pamoja katika kipindi hiki ambacho wamemaliza masomo" Alisema Bw. Nassoro
Amezitaja shule ambazo zitashiriki katika mashindano hayo kuwa ni Alpha High School, Ahmes Secondary School, Crown Secondary School, Rosmin Secondary School,

Amezitaja nyingine kuwa ni Marian Boys Secondary School, St. Joseph Boys Secondary School, Heritage Secondary School na Abbey Boys Secondary School.

No comments