Breaking News

TARURA DAR YAANZA KUTEKLEZA MAAGIZO YA WAZIRI BASHUNGWA

Mhandisi Geofrey Mkinga akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na mtandao huu hivi karibuni.

Dar es salaam:
WAKALA wa Barabra za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa ambaye aliagiza kuwepo kwa ushirikishwaji wa viongozi wa ngazi za chini kunzia Kata unapotekeleza majukumu yake.

Hayo yalibainishwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga alipokuwa akizungumza na mtandao huu hivi karibuni ambapo alisema kuwa wameanza vikao vya kuwashirikisha viongozi kuanzia ngazi ya chini kuelekea maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Hata hivyo alisema kuwa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam vile vile kwa sasa wanaendelea na utekelezaji wa bajeti ambayo ilipitishwa kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

“Tupo kwenye maandalizi ya bajeti nyingine sasa ya 2022/2023 ambapo kama mnavyojua vikao vya Bunge vinatarajiwa kuanza mwezi wa 4. Kwahiyo sisi tumeendelea kufanya vikao vile vya chini kuanzia ngazi ya Kata, Baraza la Madiwani, lakini pia ngazi ya Bodi ya Barabara ya Mkoa ambayo ndiyo inadhamana ya kupitisha barabara ya TARURA pamoja na TANROADS kwa ngazi ya Mkoa, kabla sasa haijapelekwa kwa ngazi ya Wizara ili kupeleka Bungeni. Kwahiyo tupo kwenye ngazi hizo kwa sasa,”.

“Kuanzia ile Disemba na hii Januari, kwa mfano Mh. Waziri wa Tamisemi alituagiza kwamba Tarura tuhakikishe kwamba tunawashirikisha Madiwani katika kuhakikisha kwamba mapitio ya zile bajeti na mapendekezo ya vile vipaumbele tunawashirikisha wao. Na ndiyo zoezi ambalo tumeendelea nalo,” alisema Mhandisi Mkinga.

Alisema kuwa hadi sasa wamekwishafanya vikao vya ushirikishwaji katika Wilaya za Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni ambapo alieleza kuwa lengo ni kuwaonesha rasimu ya bajeti.

Mkinga alisema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu vyanzo vyao vya fedha ni vitatu ambavyo ni kutoka Serikali Kuu, Halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo ikiwemo miradi ya DMDP ambayo hutokana na mikopo au ufadhili.

“Kwa hivyo tunavyowashirikisha hawa madiwani wanaona, uwezo wa Serikali katika kuhudumia zile bajeti kwa maana ya Serikali Kuu, lakini pia na wao wanapata wasaa wa kuona sasa na wao watachangia kiasi gani. Tumefanya hivi kabla ya vikao vyao vya kibajeti havijaanza ili sasa waone wanatupangia sisi nini, kwa sababu zile barabara nyingi zipo kwao".

Mhandisi Mkinga alieleza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una mtandao wa barabara nyingi ambapo alieleza kuwa katika mtandao huo zaidi ya asilimia 50 una hali mbaya huku asilimia nyingine 50 ukiwa na hali nzuri na wastani.

Hivyo alisema kuwa wanahitaji ushirikiano mkubwa na viongozi hao wa Halmashauri kwa maana ya madiwani ambao ndiyo wenye fedha.

Vila vile Mhandisi Mkinga alisema kuwa ushirikishwaji huo unawasaidia kujua barabara gani ni muhimu ambazo zinapaswa kupawa kipaumbele katika matengenezo.

“Kwa hiyo lazima tushirikiane nao kwa kuwa wao ndiyo wanajua uhitaji wa barabara kwani wanajua ni barabara ipi ambayo wananchi hutumia. Kwa hiyo katika dhana nzima ambayo Mh. Waziri alitusisitiza tuifanye kwa maana ya Mh. Ummy Mwalimu kabla na kwa sasa Mh. Bashungwa juzi wakati anaonga na TARURA alitusisitiza kwamba lazima tushirikiane, kwa Dar es Salaam tumeshaendela kushirikiana,” alisisitiza Mhandisi Mkinga.

Akizungumzia kuhusu mfumo wa ukusanyaji mapato ya maegesho ya vyombo vya moto (magari) kwa njia ya kielekroniki, alisema kuwa ulipoanza kutumika kwa mara ya kwanza kulijitokaza changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa elimu kwa wananchi juu ya mfumo huo.

Ambapo alieleza kuwa pamoja na changamoto nyingine zilizojitokeza wameendelea kuhakikisha wanaziondoa ili mfumo huo uendelee kutumika kwa ufanisi pasipo malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi.

Aliwahakikishia wananchi kuwa ndani ya miezi mitatu kuanzia mwezi Desemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu waliyopewa kufanyia kazi changamoto hizo, zitakuwa zimekwisha.

Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyokuwepo juu ya viwango vya faini ambavyo vilikuwa vikubwa, alisema kuwa Serikali iliona ni vyema wavifanyie maboresho.

“Sababu mwanzo ilikuwa kama hujalipa ndani ya siku saba, lile deni lako la msingi kama ni Sh. 1,000 baada ya ile siku ya saba dani linakuwa sh.2,000 na ikienda siku ya 14, haujalipa lile deni lako unakuwa na deni la sh.30,000 kwa hiyo na hiyo 2,000 ulikuwa unapaswa kulipa jumla ya sh.32,000,” alisema Mhandisi Mkinga.

Hivyo alisema kwamba suala hilo limeangaliwa sambapo Serikali imerekebisha muda wa kulipa ambapo anatakiwa mtu kulipa ndani ya siku 14 badala ya siku 7 ambapo uhuru wa muda wa mtu kulipa umeongezwa.

Mhandisi mkinga alisema jambo la pili, imeondolewa faini ya sh.30,000 ambapo imeshushwa hadi sh.10,000. Kwamba mtu akishindwa kulipa ndani ya siku 14, siku ya 15 atapaswa kulipia sh.11,000.

“Hakuna ile 1,000 kuwa 2,000 na ile sh.30,000 kwa hiyo Serikali imeshusha hapo, lakini pia imeongeza muda. Kwahiyo mpaka ukafike kulipa shilingi 10,000 maana yake wewe umetaka, wewe ni mkaidi, na inaeleweka kwamba maegesho yote mjini yanalipiwa hakuna egesho la bure,” alisema Mhandisi Mkinga.

Aidha alisema kuwa baada ya kufuatilia walibaini kuwa malalamiko mengi yalikuwa yanatolewa na watu ambao walikuwa wanapaki siku nzima hususani watoa huduma ambapo walikuwa wakikatwa sh.4,500.

Hivyo ili kuondoa mamalamiko hayo wameamua kuanzisha huduma ya kifurushi ambapo mtu anaweza kununua kwa sh.2,500 na kupaki gari lake kwa siku nzima.

Alisema kuwa baada ya kushusha viwango hivyo walitangeneza sheria ya kuendana na jambo hilo, ambapo Desema 3 mwaka jana waliletewa sheria na kanuni ndogo ambapo ndani yake waliboresha muda wa ukusanyaji.

“Kanuni ndogo inasema muda wa ukusanyaji ni kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni, lakini pia kwa maana ya mazingira ya Dar es Salaam yalivyokaa na ukubwa wake, na watu wanaofanya kazi wanatoka sehemu mbalimbali, kwenye sheria tumetoa mwanya wakala anona muda sahihi upi wa kuanza. Kwa sasa ni saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni,” aliseme Mkinga.

Mhandisi Mkinga alitoa tahadhari wa watumiaji wa vyombo vya moto kwamba baada ya maboresho hayo ya muda wa kulipa, wapo watu ambao wameacha kufanya malipo yao jamboa ambalo ni sawa na ukaidi.

Aliwataka wenye madeni wote kufanya malipo kabla hawajaanza kuawakamata kwani taarifa zao wanazo na hakuna hata mmoja ambaye atakwepa isipokuwa kulipa tu.

No comments