Breaking News

PROF LIPUMBA AFUNGULIWA MASHTAKA AKITUHUMIWA KUKIUKA KATIBA YA CHAMA

Makamu mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Zanzibar, Musa Haji Kombo pamoja na wanachama wengine wa chama hicho wamemfungulia kesi mwenyekati wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba. 

Akizungumza jijini dar es salam amesema kesi hiyo namba 633/2021 iliyofunguliwa mahakama kuu ya Tanzania ambayo inatarajia kutajwa machi 24 mwaka huu chini ya jaji Ephery Kiswaga.

"Nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia keshi mwenyekiti wa chama taifa kufatia yakiuka katiba ya chama mara kwa mara jambo linalopelekea kutokuleta taswira nzuri katika kujenda taasisi zaidi ya kuidhohofisha" Alisema Kombo.

Alisema kufatia hali hiyo akiwa kama moja ya waasisi wa chama hicho ameshawishika kwenda mahakamani kumtaka mwenyekiti huyo kutoa ufafanuzi na ikiwezekana kutengua baadhi ya maamuzi ambayo ameyafanya.

Amezitaja sababu ambazo zimemsukuma kufungua kesi hiyo kuwa ni matumizi mabaya na kuyokuhusisha vingozi wenzake katika matumizi ya malimbikizo ya ya fedha za ruzuku zaidi ya Bilioni 1, kumvua uanachama Anbas Juma Muhunzi ambaye alikuwa makamu mwenyekiti kabla yake.

Amezitaja nyingine kuwa ni kutomshirikisha makamu wa chama Zanzibar katika teuzi za wakurugenzi kama katiba inavyoelekeza, kuvunja kamati tendaji ya kinondoni kwa sababu ya kumlinda mtu mmoja pamoja na kuendesha chama kinyume na mapendekezo yaliopitishwa na mkutano mkuu wa mwaka 2019.

No comments