Breaking News

NAIBU WAZIRI ARDHI MH. RIDHIWANI KIKWETE AHANI MSIBA WA MKE WA RC SHIGHELA

Na Andrew Chale, Dar es Salaam.
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Ridhiwani Kikwete (MB),  mapema leo Januari 22, ameungana na viongozi wengine mbalimbali kuhani msiba wa Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shighela, msiba huo upo Salasala, Dar es Salaam.

Mh. Ridhiwani Kikwete amefika nyumbani kwa RC Shighela na kumpa pole ikiwemo salamu za rambirambi kutoka kwa Wananchi wa Jimbo la Chalinze Jimbo ambalo linapakana na Mkoa wa Morogoro.

Awali Mh. Ridhiwani Kikwete akitoa salamu zake alisema:

"Inna Lillahi wa inna ilayhi rail'un. Nampa pole Mhe. Martin Shighela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kwa kufiwa na mke wake Bi. Magdalena Anney Layda. 

Mungu ampe subira, uvumilivu na nguvu katika kipindi hiki kigumu kwake na familia nzima." Alisema Mh Ridhiwani Kikwete. 
Aidha, katika tukio hilo pia viongozi mbalimbali walikuwepo akiwemo Waziri wa Madini, Mh. Dotto Biteko pamoja na viongozi wengine Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakari Kunenge, lakini viongozi wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Katibu Mkuu Mwenezi Daniel Chongolo, Katibu wa NEC, Shaka na wengine.

Msiba huo wa Mke wa Shighela ulitokea usiku wa kuamkia Januari 20 mwaka huu  katika Hospitali ya Aghakhan,  Dar es salaam alikokuwa amelazwa.
Mwili wa marehemu mke wa Shighela unatarajiwa kusafirishwa leo jioni kuelekea Shinyanga kwa shughuli za mazishi.

No comments