Breaking News

TANAPA YANG'ARA MAONESHO YA UTALII YA FITUL NCHINI HISPANIA

Ushiriki wa Hifadhi za Taifa Tanzania  katika Kongamano la Maonesho ya Kibiashara Kimataifa la FITUR nchini Hispania limeendelea kuwavutia wengi kupanga kutembelea Hifadhi za Taifa hivi karibuni.

Afisa kutoka TANAPA, Bw. Jerome Ndanzi anayeshiriki maonesho hayo amesema Mawakala wa Utalii waliotembelea Banda la TANAPA wameridhishwa na maelezo ya vivutio vya utalii katika Hifadhi za Taifa na kuweka miadi ya kuvitembelea hivi karibuni.

Tanzania  imekuwa na vivutio vingi vya Hifadhi zake za Taifa kama vile Hifadhi za Serengeti, Mikumi, Ruaha, Tarangire, Mkomazi, Nyerere na zingine nyingi ikiwemo Mlima Kilimanjaro.

Na Mwandishi Maalum, Hispania

No comments