Breaking News

NAIBU WAZIRI MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAFARIJI WALIOPATA MAAFA CHALINZE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Mhe. Ridhiwani Kikwete  (wa pili kulia) akioneshwa moja ya jengo la madarasa yaliyoezuriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua hivi karibuni katika Mji mdogo wa Bwilingu, Chalinze. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhan Possi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Mhe. Ridhiwani Kikwete  (kushoto) akioneshwa moja ya nyumba iliyoezuliwa paa na upepo mkali ulioambatana na mvua hivi karibuni katika Mji mdogo wa Bwilingu, Chalinze. Katikati ni Diwani wa Kata ya Bwilingu, Mhe Nassa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Mhe. Ridhiwani Kikwete  na viongozi wengine wa Halmashauri ya Chalinze wakiangalia uzio wa muda katika Halmashauri hiyo ambao nao ulipata athari kufuatia kadhia hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Mhe. Ridhiwani Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Makombe waliopatwa na kadhia ya mvua na upepo mkali ndani ya jimbo hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Mhe. Ridhiwani Kikwete  katika maeneo yaliopatwa athari ya mvua hiyo wakati wa ziara yake ya kutoa pole kwa wananchi wa Kijiji cha Makombe.

Na Andrew Chale.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB) mapema leo Januari 23,2022 amefanya ziara fupi na kutoa mkono wa pole kufuatia majanga ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha hivi karibuni na kuezua mapaa ya nyumba na  Madarasa katika Kijiji cha Makombe na Mji mdogo wa Bwilingu ndani ya Jimbo hilo la Chalinze, Mkoani Pwani.

Akiwa katika eneo hilo,Mhe. Ridhiwani Kikwete alipata kutembelea Wanananchi na kutoa pole huku akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Diwani wa Bwilingu Mhe. Nassa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze. 

"Nnefanya ziara fupi kijiji cha Makombe na Mji wa Bwilingu kutoa pole kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali kuezua paa za Nyumba na madarasa, na kuwaacha wananchi katika tabu kubwa.

Kwanza natoa pole kwa Wananchi wote waliopatwa majanga mimi kama Mbunge wao nimeguswa na kufanya ziara fupi kujionea hali halisi.

"Lakini pia nikiwa kama kiongozi ninayemwakilisha Rais, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa niaba yake nitoe pole za dhati kwa wananchi wa Jimbo langu la Chalinze  na maeneo yote ya Tanzania waliokumbwa na kadhia hii ya athari iliyotokana na mvua na upepo mkali, tumeona kule Kibiti pia nyumba na madarasa yameezuriwa na upepo na hata kusababisha maafa na vifo kwa watoto". 

Aidha, Mhe. Ridhiwani Kikwete aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali chini ya Rais,  Samia Suluhu Hassan ipo bega kwa bega na watahakikisha wanapatiwa misaada na mambo mengine yaendelee.

"Tumekubaliana kuwa ndani ya wiki hii Shule iwe imerudi katika hali yake na kwa wananchi taratibu zinafanywa kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo  vyakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu." Alisema Mhe Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete. 

Aidha, Naibu Waziri Mhe. Ridhiwani Kikwete ameweza kuchangia shilingi Milioni 5 mfuko wa Maafa ili kupunguza makali ya Madhara hayo.

Mvua hiyo iliyonyesha hivi karibuni imeweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo nyumba na majengo ya madarasa  kuezuriwa paa na kwingine kubomoa kuta na mazao ya miti.

No comments