Breaking News

ZIARA YA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM TAIFA KASKAZINI PEMBA

Katibu  wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameshiriki  katika ukaguzi wa ujenzi wa Ukingo wa bahari  kuzuwia eneo la bahari isingie kwenye makazi ya wananchi, ikiwa ni utekelezaji wa Ibara 192 ya ilani uchaguzi 202/2025.

Ujenzi huo umefikia asilimia 80 umegharimu jumla ya Shillingi millioni 300  ambapo hadi kukamilika T. Shs 510,286,500 zitatumika chini ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. 
Aidha Ameshiriki katika ujenzi wa Taifa Tawi la CCM  Chimba na kisha  kuzungumza na wanachama na wananchi  katika shina no 2.

Ziara hiyo inaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Cde Daniel Chongolo  kisiwani Pemba kwa siku mbili.



No comments