Breaking News

TFS YAPEWA MBINU KUMALIZA MALALAMIKO YA WANANCHI KWENYE MISITU

Dar es salaam. 
Hayo yamejiri jumapili tarehe 23/01/2022 kwenye kikao kazi cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja kilichofanyika ofisi ya TFS Makao Makuu Mpingo house jijini Dar es salaam. 

Akipokea taarifa juu ya malalamiko ya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka Msitu wa Sayaka uliopo kati ya Wilaya ya Magu na Wilaya ya Busega, Mheshimiwa Masanja ametoa mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa na TFS kumaliza migogoro kwenye Misitu.

"Hii migogoro kwenye Misitu na Wananchi sasa basi, tumieni mbinu rafiki,itisheni mihadhara mtoe elimu watu waelewe, fanyeni uwezeshaji kwa wananchi waliopo kwenye maeneo husika, anzeni miradi ya kupanda miti kwenye mipaka, wachimbieni mabwawa kwa ajiri ya Mifugo yao,fanyeni haya kwa haraka kwa kuwashirikisha wananchi wataelewa wataachia mipaka ya Misitu "Mh Masanja.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt Francis Michael ameelekeza TFS kupitia ramani za maeneo ya Misitu yenye migogoro ya mipaka kwa kushirikiana na Idara ya Aridhi ili kuanza utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri .

"kwa hiyo Profesa fuatilia ramani za maeneo ya Misitu yenye migogoro, shirikiana na Kamishina wa Aridhi ili iwe rahisi kuzipata kisha utekelezaji uanze mara moja Dkt Francis.
Katika kikao kazi hicho Kamishina wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo amewasilisha taarifa ya malalamiko ya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka Msitu wa Sayaka ambapo amemhakikishia Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa atafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili kuwawezesha wananchi kuelewa na kushiriki kikamilifu katika Uhifadhi wa Misitu.
 

No comments