Breaking News

BI MAIMUNA SAIDI AJITOSA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE KUPITIA CHAMA CHA ADC

Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw Doni Mnayamani akimkabidhi fomu Bi. Maimuna Said kuomba chama hicho kumpitisha kugombea nafasi ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es salaam.
Bi. Maimuna Said akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu kuomba chama hicho kumpitisha kugombea nafasi ya Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es salaam.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw Doni Mnayamani akimkabidhi fomu Bi. Maimuna Said akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya utaratibu wa chama kwa wanachama wa chama hicho kugombea nafasi ya Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es salaam.
Bi. Maimuna Said akionyesha fomu ya kuomba chama hicho kumpitisha kugombea nafasi ya Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Mwanachama wa Chama Cha Alliance For Democratic Change(ADC) Bi Maimuna Said amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea  nafasi ya Usipika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu na Kaimu Naibu katibu Mkuu Bara Doni Mnyamani makao makuu ya chama buguruni jijini Dar es salaam Bi. Maimuna amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kulifanya bunge kuwa mhimili wenye hadhi na kurudisha imani watanzania pamoja na kurejesha hadhi ya chombo hicho kwa kutimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali, kuikosoa na kuishauri.

"Nina nia na sababu tatu madhubuti kugombea nafasi hii kwani kwanza ni haki yangu ya kikatiba kugombea, pili nataka kwenda kulifanya bunge kuwa mhimili wenye hadhi katika nchi yetu na sababu ya tatu kukuza na kuongezea imani ya watanzania kuhusu chombo chao kwa kutekeleza majukumu yake kama kuisimamia, kuikosoa na kuishauri serikali" Alisema Bi. Maimuna.

Alisema ayo ni baadhi ya masuala mengi ambayo  nitayasimamia endapo nitapitishwa na chama changu cha ADC na wabunge kunichaguwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Awali Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw Doni Mnayamani amesema hadi sasa mwanachama mmoja pekee ndio aliejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kukiwakilisha chama kugombea nafasi ya Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado chama hicho kinaendelea kupokea maombi ya wanachama wanaotaka kujitokeza kuchukua fomu.

"Hadi sasa mgombea aliejitokeza ni mmoja ambae ni Bi Maimuna Said, ikumbukwe kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 aligombea ubunge katika jimbo la Kilindi Mkoani Tanga" 

Bw. Myamani aliongeza kuwa chama bado kinaendelea kupokea wanachama wenye nia ya kugombea nafasi hiyo hadi tarehe 24 mwezi huu ambapo kikao cha kamati tendaji kitakaa ili kuteua jina moja la mgombea ambae jina lake tutalipeleka tume ya taifa ya uchaguzi kwa ajili ya taratibu zingine.
 

No comments